TANGAZO


Friday, August 19, 2016

UME YA MIPANGO YATOA MAFUNZO YA MPANGO WA MAENDELEO

Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy akifafanua kwa Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara kuhusu umuhimu wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo,Bw.Hassan Abbasi na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa. (Picha zote na Fatma Salum-Maelezo)
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Bw. Hassan Abbasi akifungua Mafunzo kwa Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mambo ya kuzingatia katika Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo ili kuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma. Katikati ni  Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa. 
Mchambuzi Sera Kutoka Tume ya Mipango, Bi. Lilian Wawa akiwasilisha mada kwa Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara kuhusu Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, leo Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa akiongea na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara (hawapo pichani) wakati wa Mafunzo kuhusu Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni  Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy na Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Bw. Hassan Abbasi. 
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara wakifuatilia mafunzo kuhusu Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo yaliyotolewa kwao na Tume ya Mipango, Leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment