Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TAGLA), Bw.Charles Senkondo (wa kwanza kulia), akimkabidhi kitabu cha maswala ya TEHAMA Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejemanti, Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Bi.Susan Mlawi (kushoto), katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Ajira, Daudi Xavier (aliyesimama), akiwasilisha mada mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejemanti, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani), katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick
Mfugale akichangia mada katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Watendaji
Wakuu wa Wakala za Serikali uliofanyika
jijini Dar es Salaam.
Na
Sheila Simba-Maelezo
Mawasiliano ya TEHAMA yametakiwa kuboreshwa ili kusaidia Serikali katika mchakato wa kuhamia
Dodoma kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Magufuli ili kutekeleza mpango uliowekwa na Baba waTaifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza hayo katika ufunguzi wa kikao cha
kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali (fcega), Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi
ya Rais, Menejemanti, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bibi Susan
Mlawi alisema kuwa mawasiliano hayo ya TEHAMA yanapaswa kupewa kipaumbele katika utendaji kazi wa Serikali ili kupata watumishi
bora.
“Matumizi ya teknolojia ya Tehama
yatasaidia Nchi kufikia maendeleo haraka na kupunguza gharama za watu kusafiri kwa ajili ya
kwenda kwenye vikao vya kazi kama zifanyavyo nchi nyingine,” alisemaBibi Susan.
Aidha, Bibi Susan ameongeza kuwa wakala wa Serikali watumie mafunzo kwa njia
ya mtandao (TAGLA) kwa kuwa wana uwezo wa kutoa mafunzo yatakayoisaidia Serikali katika mawasiliano na taasisi zake hasa katika mkutano masafa (telle
conference)
Mbali na hayo Bi. Susan amesema kuwa Kuongeza Ufanisi katika Mchakato wa Ajira kwa Kutumia Teknolojia”
ni mada muafaka inayoleta chachu ya
kuongeza ubunifu na kufanyakazi kwa ufanisi zaidi hususani katika taasisi za Kiserikali.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya
ajira Daudi Xavier,alisema kuwa wanatumia teknolojia katika kupashana habari, upokeaji wa maombi
ya ajira na utunzaji wa taarifa za waombaji fursa za ajira, katika kufanya mikutano ya
kiofisi kwa kutumia mkutano masafa na kupunguza gharama za matangazo.
“Tunatumia Tehama sana katika kazi zetu na hii imetusaidia kubaini wanafunzi wadanganyifu kwa upande wa vyeti kwa kufanya mawasiliano na taasisi za elimu kupata taarifa za watu wanaotuma maombi
ya kazi”alisema Bw.Daudi.
Mbali na hayo pia Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia
ya Mtandao (TAGLA), Bw.Charles Senkondo alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kubadilishana mawazo na kutatu changamoto zinazozikabili taasisi mbalimbali za Kiserikali katika maswala
ya teknolojia.
“Teknolojia sasa hivi imekua kwa kiasi kikubwa na tunaweza kutumia tehama katika kazi zetu za kila siku na sisi
TAGLA tupo tayari kusaidia katika kuboresha hilo ili kurahisisha mawasiliano na kusaidia kujifunza teknolojia” alisema Bw.Senkondo.
Kwa upande wake Mkurengezi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA), Bw.
Hiiti Sillo alisema kuwa teknoloji hiyo isaidie katika kupata wakaguzi bora
wa vyakula na dawa kwa maendeleo ya Taifa ili kusaidia jamii kuondokana na madhara yatokanayo na bidhaa zenye sumu.
“Naamini kupitia taaluma hii ya
kisasa itasaidia sana katika kufanikisha ufanyajikazi wetu katika kukagua na kuthibitisha bidhaa zilizo
bora kwa matumizi ya Watanzania”alisisitiza, Bw.Sillo.

No comments:
Post a Comment