TANGAZO


Sunday, August 14, 2016

SIMBA YA TANZANIA, URA YA UGANDA NGUVU SAWA MCHEZO WA KUJIPIMA NGUVU UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Mashabiki na wanachama wa Simba wakifuatilia mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu yao hiyo dhidi ya URA ya Uganda, mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoshana nguvu na hivyo kufungana bao 1-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ubao wa matokeo ukionesha Simba ya Tanzania bao 1 na URA ya Uganda bao 1. Mabao hayo yalipatikana katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo. 
Ibrahim Ajibu wa Simba (kushoto), akiwania mpira na Kowaya Fahad wa URA ya Uganda.
Ibrahim Ajibu wa Simba (kushoto), akimtoka Kowaya Fahad wa URA ya Uganda katika mchezo huo. 
Hadi dakika ya 44 kuingia dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza matokeo yalibaki Simba bao 1 na URA bao 1.
Nembo ya Simba na ya URA kwenye ubao wa matangazo.
Jamal Mnyate wa Simba akiwatoka wachezaji wa URA wakati wa mchezo huo. 
Laudit Mavugo wa Simba akiudhibiti mpira katikati ya wachezaji wa URA wakati wa mchezo huo. 
Makocha wa Simba wakizungumza jambo na msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara (kushoto), mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Makocha wa Simba (katikati) na wa URA (kushoto), wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo. Kulia ni msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Haji Manara (kushoto), Alfred Lucas.
Makocha wa Simba (katikati) na wa URA (kushoto), wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo. Kulia ni msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Haji Manara (kushoto), Alfred Lucas.

No comments:

Post a Comment