Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi,Dkt.
Leonard Chiriho akimzungusha Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara
wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Lin Zhiyong (katikati) alipotembelea
Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) jana Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi
huyo alitembelea chuoni hapo ikiwa ni ziara ya tathmini kama chuo hicho
kinakidhi kupata ufadhiri wa China katika mpango wake wa kujenga Vyuo Vikuu
Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi,
Profesa Zacharia Mganilwa.
Na Frank Shija,
MAELEZO
14/08/2016
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji
(NIT) kuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vitakavyo jikita katika fani za
Usafirishaji vitakavyojengwa Barani Afrika kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa China.
Hayo yamebainishwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Dkt. Leonard
Chamuriho alipokutana na Mwakilishi Mkuu wa masuala ya Uchumi na Biashara
kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Bwana Lin Zhiyong wakati
wa ziara ya kufanya tathmini juu ya uwezo wa NIT katika utoaji wa elimu ya
Usafirishaji na namna ya kuweza kukisaidia chuo hicho.
Katika ziara hiyo
Katibu Mkuu huyo amemuhakikishia Mwakilishi Mkuu wa masuala ya Uchumi na
Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuwa NIT iko imara na inayo
mipango kabaambe kwa ajili ya upanuzi wa chuo hicho utakao enda sambamba na
kuongezeka kwa Programs zitakazokuwa zikifundishwa.
“Kutokana na urafiki
wa muda mrefu tulionao baina yetu na China ni imani yangu kuwa Chuo hiki
kitakuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji vitakavyojengwa kwa
masaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China barani Afrika kama ambavyo Rais
wan chi hiyo alivyo dhamiria wakti wa mkutano huko Afrika ya Kusini” Alisema
Dkt. Chamuriho.
Ni dhahiri kuwa wataalamu
wa masuala ya usafirishaji wanatakiwa kwa wingi kwani ukuaji wa Sekta hiyo
unaenda kwa kasi hali kadhali Jiografia ya nchi yetu inatoa fusra kwa Tanzania
kujenga miundombinu ya usafirishaji kama vile Barabara na miundombinu ya Reli,
Viwanja vya Ndege ili kuunganisha na Bandari.
Mpango huo umekuja
katika wakati muafaka kwani utasaidia kuongeza idadi ya waataalam katika sekta
ya usafirishaji kwa kuwa wanafunzi wengi zaidi watajiunga na masomo mbalimbali
yatakayofundishwa katika chuo hicho kitakapo kamilika.
Mhandisi Profesa
Zacharia Mganilwa ni Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji, anasema kuwa wao
kama uongozi wa chuo wanao mpango mahususi wa kufanya maboresho makubwa ya Chuo
hicho ili kiweze kukidhi mahitaji halisi ya Sekta ya usafirishaji hapa nchini
kwa sasa.
“Sisi kama Taasisi
tumejipanga kuhakikisha tunafanya maboresho ya Chuo chetu ili kiendane na hali
halisi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji hapa nchini, katika mpango huo
tumenuia kuanzisha Shule tano zitakazo jikita katika nyanja za Shule ya Uhandisi
na Teknolojia, Shule ya Teknolojia ya Anga, Shule ya Usafirishaji na
Logistic,Shule ya Elimu, Hisabati na Kompyuta na Shule ya Biashara NIT”.
Mhandisi Mganilwa.
Aliongeza kuwa kutokana
na mpango huo NIT inalo maeneo yakutosha na kukidhi mahitaji ya utekelezaji wa mpango
huo kwani ina jumla ya ekari 46 katika eneo la sasa ambapo kuna ardhi ekari 46
ambapo kati ya hizo ni asilimia 30 tu ndiyo iliyotumika hadi sasa, pia chuo
kimefanya utaratibu wa kupata eneo jingine la ekari 1600 katika wilaya ya
Bagamoyo mkoani Pwani.
kizungumza wakati wa
ziara hiyo ya kufanya tathmini ya Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na
Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong
ameonyesha imani kwa Chuo hicho na kuahidi kusaidia katika kuhakikisha kinakuwa
miongoni mwa Vyuo hivyo Vitano vilivyoahidiwa na Rais wao.
Aliongeza kuwa
kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo hadi kufikia mwaka 2015 Tanzania itakuwa
nchi ya uchumi wa kati.
“Nimeshawishika na
niliyojionea hapa naweza kusema Serikali yetu itakuwa tayari kusaidia program
mbalimbali zilizopo hapa na kutokana na urafiki wa kihistoria uliopo
nawahakikishia kuwa NIT itakuwa miongoni
mwa Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika vitakavyojengwa na
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kama ambavyo Rais wetu alivyo ahidi wakati
wa Mkutano Jijini Johannesburg, Afrika Kusini”.Alisema Zhiyong.
Zhiyong aliongeza
kuwa ujenzi huo wa Vyuo hivyo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka
mitatu.
Ziara hiyo ya
Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu
wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya tathmini
juu ya program zinazofundishwa, rasilimali watu na miundombinu kwa maana ya
eneo.
No comments:
Post a Comment