Afisa Mtendaji Mkuu wa Tinny Entertainment kutoka Nigeria Arokodare Timilehin akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE (wa tatu kutoka kushoto), leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.
Msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE kutoka Nigeria akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake katika Vyombo vya Habari inayoratibiwa na Kampuni ya Uhusiano wa Umma ya LAS Consultancy ya Jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mwanzilishi wa Kampuni ya LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana, Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina ya uongozi wa LAS Consultancy walipokuwa wakimtambulisha msanii kutoka Nigeria Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE ambaye yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kutembelea Vyombo vya Habari.
Msanii
Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE kutoka Nigeria akimkabidhi mfano wa hundi
yenye thamani ya shilingi milioni moja kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea
watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule(kushoto) leo Jijini Dar
es Salaam Katikati ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.Msanii
hyo yupo nchini kufuatia ziara yake kwa Vyombo vya Habari inayoratibiwa na
Kampuni ya Mahusiano ya Umma ya LAS Consultancy.
Na
Sheila Simba, Maelezo
MSANII wa muziki kutoka nchini Nigeria Omo Alhaji,Jagabana maarufu YCEE,ametoa msaada
wa shilling million 1,kwa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira
magumu cha Kigamboni Community Center(KCC).
Akizungumza
katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo jijini Dar es salaam mratibu wa
ujio wa msanii huyo bi Salha Kibwana amesema kuwa msanii YCEE ametoa msaaada
huo katika kituo hicho kwa lengo la kusaidia watoto hao ili kujipatia mahitaji
maalum ya kila siku wawapo kituoni hapo.
“Ametoa
msaada huo kutokana na faaida anayopata katika kazi zake usanii ili kukuza
vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu wa elimu kwa jamii hasa ya watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi,”alisema Salha.
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa kituo hicho Mbwana Msangule,amesema
kuwa kituo chake kinalea watoto hao ili kuwasaidia kuondokana na maisha magumu
yanayowakabili.
“msaada
huu utasaidia sana kwasababu kituo kina watoto 14 wanaoishi kituoni hapo na
wengine wanakuja na kurudi makwao,na nashukuru sana kwa msaada huu kwani ni
sanii wa kwanza kutoka msaada,nawaomba
pia wasanii wa ndani kijitokeza kutoa msaada”alisema Mbwana.
Kwa
upande msanii huyo amesema kuwa amekuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na
kuonana na wasanii wengine wakubwa wa Tanzania huku akiwataja Diamond na Ali
Kiba,ameongeza kuwa amefurahi pia kuktana na mashabiki wake ambao amekua
wakichati kupitia mitanzandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment