Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia)
na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi
madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na
viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale.
Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang'wale.
Utengenezaji wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano.
Fursa ya ajira iliendelea kusambaa kwa dereva wa trekta Bw ,Machibya aliyepata tenda ya kusafirisha Madawati kwenda katika shule zilizokusudiwa kupata Madawati hayo.
Lakini pia wakati wa shughuli za utengezaji wa Madawati hayo mafundi walihitaji kupata chakula na hii pia ikawa Fursa kwa Mama Nitilie Devotha Sonda wa Sonda ambaye alikuwa akitoa huduma ya chakula kwa mafundi hao.
Na Dixon Busagaga
wa Michuzi Blog, Kanda ya Kaskazini
MGODI wa dhahabu
wa Bulyanhulu umetengeneza mamia ya ajira kwa vijana na wanawake wanaoishi
maeneo mbalimbali mkoani shinyanga na Geita kupitia mpango wa kutengeneza
madawati elfu sita katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo yenye thamani ya
shilingi milioni 200.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti vijana wamesema neema ya kujiingizia vipato kwa kushiriki
kwenye shughuli mbalimbali katika zoezi la kutengeneza madawati imebadili
maisha yao hasa katika msimu huu wa kiangazi ambao wengi wao ajira zao
zimesimama kwani walio wengi wanategemea mvua kwenye ajira yao ya msingi ya
kilimo.
“Tunashukuru sana
msimu huu wa kiangazi, tumepata nafasi ya kupata kazi za ambazo zinatupatia
kipato kupitia utengenezaji wa madawati, mimi hapa ni fundi chuma, nachomelea
vyuma na kazi yangu hii huku vijijini wateja ni wachache sana, muda mwingi huwa
tuko doro kwenye kijiwe chetu lakini sasa hivi tuna kazi nyingi sana za
kutengeneza madawati hapa imebidi niajiri vijana wengine watano kuweza
kunisaidia kukamilisha kazi ya kuunganisha vyuma kwa ajili ya madawati mia tano
ambayo tumepata tenda na Kampuni iliyoshinda tenda ya kutengeneza madawati kwa
gharama ya mgodi wa dhahabu ya Bulyanhulu.” Anasema Abbas Mbua mkazi wa kata ya
Msalala wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.
“Sisi wapiga msasa
tunajipatia shilingi elfu kumi na tano kwa kila dawati 5 hii si haba, kiasi
hiki kimenisaidia sana maana sikupata vizuri mazao mwaka huu kwa hiyo pesa
niliyoingiza kwenye kazi ya kupiga msasa imebadili kabisa hali halisi nyumbani,
nimenunua gunia za mahindi, maharage na mchele, hali imetulia kwa kweli siwezi
kusema uongo” anasema Maige Deus mkazi wa Kahama.
“Ninaiomba sana
serikali yetu iendelee kuvumbua miradi mingine ili sisi vijana tuendelee
kuchapa kazi, maana vinginevyo tunakaa vijiweni kazi hamna, lakini mradi huu wa
madawati ulivyokuja hatuna hata muda wa kuvuta sigara, tuko bize kutwa nzima
tunatengeneza madawati, hapa mimi ndiyo fundi mkuu kwenye hiki kiwanda naunganisha
mbao na kuhakikisha madawati yako vizuri kwa ajili ya wanafunzi.” Anasema Abdul
Karim Ramadhani akiwa katika kiwanda cha Zacharia and Deus Timber Supply cha
Nyang’wale mkoani Geita.
Halikadharika mama
nilitie nao wanasema si haba mradi wa kuchonga madawati umeongeza idadi ya
wateja katika migahawa yao, Devotha Sonda wa Sonda Mama Nitiliea katika kijiji
cha Msalala anasema “ Kabla ya mradi wa madawati vyakula hapa tulikwa tunapika
kidogo na wateja walikuwa ni wa kubangaiza tu lakini sasa hivi kutokana
uchongaji wa madawati vijana ni wengi sana na binafsi nimepewa tenda kabisa ya
kupikia vijana wanaotengeneza madwati na ninalipwa vizuri na kwa muda, naomba
miradi kama hii iendelee tu hadi madawati yatoshe na sisi mitaji itakuwa
imekua. Mwaka huu maswala ya ada kwa watoto, mavazi sasa ni jambo rahisi.”
Naye Mkurugenzi wa
kampuni ya kizawa ya Zacharia and Deus Timber Supply Deus Mlela iliyopo
Nyang’wale kilomita hamsini kutoka mgodi wa Bulyanhulu amesema, “Tenda ya
kutengeneza madawati mia tano kutoka Bulyanhulu kwetu tumepata faida mara mbili
kwanza imetuongezea mtaji na pili imetupa uwezo na kujulikana kwa wadau
wengine, sasa hivi tumepatiwa tena tenda na Halamashauri ya wilaya kutengeneza
madawati mengine elfu moja na kampuni nyingine imetupa tenda na madawati mia
mbili, bila kazi ya Bulyanhulu kutufungulia mlango ingekuwa vigumu kuweza
kupokea tenda hizo kwa sababu mtaji ulikuwa mdogo.
Tunaomba wadau waendelee kutuamini ili na sie tuweze kuendelea kusambaza ajira kwa vijana ambao hawana ajira.
Tunaomba wadau waendelee kutuamini ili na sie tuweze kuendelea kusambaza ajira kwa vijana ambao hawana ajira.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama amesema, “Kimsingi kuwa karibu na Mgodi wa
dhahabu wa Bulyanhulu imewafanya watu wa Nyang’wale ule uzito wa kazi ya
madawati kuwa tofauti na sehemu nyingine, japo hatujamaliza kabisa tuna
mapungufu kidogo, faida ya mradi wa madati faida yake ya kwanza ni kwa watoto
wa shule ambayo ni walengwa, wanapata madawati wake vizuri na waweze kuelewa
masomo yao vizuri, kwa njia nyingine
mpango huu umetengeneza ajira, wale watengeneza mawadaati wamepata kazi ya
kufanya na kipato, wanajipatia mahitaji wengine wananunua mifugo, kwa mfano
katika mradi huu bulyanhulu imedhamini madawati yenye thamani ya shilingi
million thethini na tano na hii pesa imezunguka kwa watu wote, mafundi
seremala, waendesha mikokoteni, mama nitilie, na wengine wengi wamejipatia
kipato na hata mitaji.”
Mwaka 2013 Mgodi
wa Bulyanhulu ulitoa madawati 1329 kwa ajili ya shule 10 za msingi zinazozunguka mgodi wa Bulyahulu.
Mwaka huu 2016
Madawati 1380 kwa halmashauri ya Msalala madawati 500 kwa wilaya ya Nyang’wale 500, madawati
2000 yatatolewa hivi karibuni kwa mkoa wa Shinyanga na pia Bulyanhulu itaipatia
dola za kimarekani elfu 6000 shule ya msingi ya binafsi ya St. Josephine
Bhakita iliyoko km 12 kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika kijiji cha
Ilogi kata ya Bulyanhulu.
No comments:
Post a Comment