Na
Sheila Simba,Maelezo
ASKOFU Dkt Charles Gadi ametoa wito
kwa wananchi kumuunga mkono Rais John Magufuli, katika mchakato wake wa kuamishia
serikali makao Makuu ya nchi Mkoani Dodoma kwani ni uamuzi wa kijasiri na
upaswa kuungwa mkono.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, Askofu Gadi amesema kuwa jitihada zinazofanywa na Rais
magufuli ni kubwa kwani jitahada zinaonekana wazi za kuimarisha mji wa Dodoma
na ili uweze kutumika kama makao makuu ya nchi.
‘’Serikali inafanya kazi nzuri
kinachotakiwa ni kumtia moyo Rias wetu ili jambo ili lifanikiwe na kuhamisha
serikali ili kutimiza mpango wa muda mrefu wa kuhamisha serikali kutoka Dar es
Salaam na kwenda Dodoma’’ alifafanua askofu Gadi.
Aidha amesema Serikali imejipanga na
inaandaa mazingira mazuri kwa watumishi wake watakao hamia huko kupata mahitaji
yote muhimu wanayohitaji,na kuongeza kuwa jambo hilo litaharakisha maendeleo
katika mikoa jirani na Dodoma.
Ameongeza kuwa imekua ni kawaida ya
baadhi ya watu kulalamika kila linapotokea jambo bila kusikiliza na kufatilia
jambo hilo kwa makini, amewaomba watanzania wasiwe watu wakulalamika kulaumu na
badala yake wawe watu wakusiliza na kufata maelekezo.
Ameongezea kuwa watafanya maombi ya
kumuombea Rais John Magufuli na viongozi
wa serikali katika mji wa buselesele wilaya ya chato mkoani Geita agosti 25
mwaka huu, kuombea mvua, amani, upendo na mshikamano baina ya serikali na wananchi
wake.
‘’Maombi haya ni ya kumuomba Mungu alifanye
taifa letu kuwa taifa bora kwa uchumi,astawi wa watuwake na linaloongoza kwa
amani na mafanikio katika kila sekta ‘’alifafanua Askofu Gadi.
No comments:
Post a Comment