Mlinzi wa timu ya Tandangongoro, Edward Mchikoba (kushoto) akikabiliana na mshambuliaji wa timu ya Mikumbi, Ramadhani Ngawina(kulia) wakati wa mchezo wa raundi ya kwanza katika mfululizo wa Mashindano ya kombe la R.P.C CUP 2016, inayoendelea kila siku kwenye Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi. katika mchezo huo timu ya Mikumbi iliibuka na ushindi wa 2-0.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Mikumbi, Patrick Charzy (kushoto)akitafuta njia ya kumtoka Kiungo mkabaji wa timu ya Tandangongoro Nasorro Abeid katika mchezo wa raundi ya kwanza katika mfululizo wa Mashindano ya kombe la R.P.C CUP 2016, inayoendelea kila siku kwenye Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi. katika mchezo huo timu ya Mikumbi iliibuka na ushindi wa 2-0.
Mlinzi wa timu ya Tandangongoro, Mohamed Mwetero (kulia) akijaribu kumzuia Kiungo Mkabaji wa timu ya Mikumbi , Saidi Masudi (kushoto) wakati wa mchezo wa raundi ya kwanza katika mfululizo wa Mashindano ya kombe la R.P.C CUP 2016 inayoendelea kila siku kwenye Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi. katika mchezo huo timu ya Mikumbi iliibuka na ushindi wa 2-0.
Wachezaji wa timu ya Mikumbi , Kiungo mshambuliaji , Ramadhani Ngawina Kushoto na Mshambuliaji Martini Chitanda (katikati) wakifukuzia kuwania Mpira dhidi ya Beki Machachali wa Timu ya Tandangongoro Mohamed Mbwatila, katika mchezo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi katika mfululizo wa Mashindano ya kombe la R.P.C CUP 2016, katika mchezo huo timu ya Mikumbi iliibuka na ushindi wa 2-0.
.Madiwani wa Kata Watingishana.
.Wachezaji wazidi kung’ara kusaka kiatu cha dhahabu
.Makocha nao wazidi kupagawa.
Na Mwandishi wa Miss Demokrasia Tanzania.
MICHUANO ya Kombe la R.P C Cup LINDI 2016, imezidi kushika kasi katika kinyang’anyoro cha kuwania ubingwa wa mwaka huu ambao umeambatana na zawadi mbali mbali zilizotolewa na baadhi ya wadhamini waliofanikisha kwa asilimia mia kufanyika kwa michuano hii mikubwa kwa mkoa wa lindi na vitongoji vyake.
timu mbali mbali zimeendelea kuonyesha uwezo mkubwa katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibunikutokana na kuchelewa kuzinduliwa kufuatia uwepo wa waziri Mkuu aliyepelekea kusogeza mbele kutokana na Maafisa mbali mbali wa Jeshi la polisi akiwepo Kamanda R.P.C Renatha Mzinga kuwa kwenye shuguli ya ziara ya Waziri Mkuu.
Mpaka kufikia leo jumla ya michezo 16 tayari imechezwa kati ya michezo 76 kabla ya kufikia fainali ya michuano hiyo ambayo mshindi atazawadiwa kombe kubwa, medali kwa wachezaji wote watakaoshika nafasi hadi ya tatu,huku kukiwa pia na zawadi mbali mbali kwa wachezaji watakaocheza vizuri, mfungaji bora, mchezaji bora chipukizi, kipa bora,na kikundi bora cha ushangiliaji.
Katika hatua hii michezo ambayo imechezwa na matokeo ni kama ifuatvyo, Mtanda A imefanikiwa kuifunga Mitandi kwa 1-0, Matopeni 1-0 Wailes, Mnazi mmoja 2-0 Mbanja, Nachingwe 0-0 Msinjaili, Rahaleo 2-1 Mtanda B, Rasibula 2-1 Tandangongoro, Mingoyo3-0 Chikonji, Mtandi 5-1 Kitumbikwela, Makonde 5-0 Mikumbi, Polisi 1-1 Matopeni, Mnazi Mmoja 4-1 Mtanda A, Msinjaili 8-0 Wailes, Mtanda(B) 2-1 Mbanja, Rahaleo 2-0 Chikonji, Rasibula 2-0 Nachingwea, Mikumbi 2-0 Tandangongoro.
Kwa Mujibu wa Waratibu na Wasimamizi wa Michuano Hiyo Afande Msafiri ambaye ni Afisa katika Jeshi la Polisi, na Mpalule Shaaban ambaye ni Mkurugenzi wa Mashujaa Radio Lindi,ambao kwa pamoja ndiyo waandaaji wa michuano hiyo,wamesema kuwa michuano hiyo inafanyika kila siku kwa michezo miwili ambapo mchana saa nane kamili kunakuwa na mchezo wa kwanza na saa kumi kunakuwa na mchezo wa pili.
Na kwamba mashindano yameendelea kuwa kuvutio kikubwa kwa wakazi wa mkoa wa lindi kutokana na wenyeji kujitokeza kuzishangilia kata zao ambazo zinawania uchampioni huo wa kombe la R.P.C Renatha Mzinga,ikiwemo kusimamia utulivu wa Uwanja, pamoja na kuhakikisha sheria zote za mchezo wa mpira wa miguu zikisimamiwa vizuri.
Jumla ya Timu 18 zinashiriki Michuano hiyo ambapo mpaka michezo hiyo inamalizika kutakuwa na Idadi ya Michezo 76 na mzunguko wa kwanza umemalizika na sasa timu zipo kwenye mzunguko wa pili baada ya timu zote 18 kucheza michezo yake ya awali huku zawadi za uwanjani za kila siku zikiendelea kutolewa kwa kwa ajili ya makocha na timu zinazoibuka kidedea.
Zawadi zingine ni kwa Makocha ambao wanapata Filimbi za Kisasa wanazoendelea kupewa na Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania pamoja na Stop Watch na wanakabidhiwa wakati wa Michezo pamoja na Furana zilizotolewa na Kampuni ya T-Mark Tanzania pamoja na Furana za GSM kwa ajili ya Waamuzi na Vikundi vya Uhamasishaji.
Kilele cha Michuano hiyo ni tarehe 25 ya mwezi wa nane ambayo itakuwa siku ya kilele cha siku ya Polisi Day.
Mashindano haya yanadhaminiwa na R.P.C Mkoa wa Lindi, Mashujaa Radio, BIG BON, T-MARK TANZANIA, GSM Wauzaji wa PIKIPIKI ZA GSM na Magodoro ya GSM, CxC Tours & Safaris, HALOTEL, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Issa Ndemanga, HAKI ELIMU,NMB, Miss Demokrasia Tanzania, MPALULEBLOGS: na PIMAK LIMITED.

No comments:
Post a Comment