Mchezaji kutoka timu ya Barclays akijaribu kuzuia mpira kutoka kwa mchezaji wa timu ya DTB wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wanamichezo kutoka mabenki mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi naodha wa timu ya DTB ngao ya hisani kwa kuwafunga mabao matatu kwa moja timu ya Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Michezo Bw. Rashid Mijuza.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na wachezaji kutoka Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Waamuzi wa michezo ya
Brazuka kibenki katika picha ya pamoja wakati wa mechi ya ufunguzi wa
mashindano ya kibenki leo Jijini Dar es Salaam.
Na
Lorietha Laurence-WHUSM
SERIKALI kupitia sera
ya Maendeleo ya Michezo inasisitiza wananchi na jamii kwa ujumla kushiriki
katika michezo ili kujenga afya, kuunganisha watu toka makundi mbalimbali bila
ubaguzi wa kidini, kisiasa, wala kiuchumi.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
wakati wa ufunguzi wa mashindano ya
Kombe la Kibenki maarufu kama Brazuka katika viwanja vya Gymkhana leo jijini
Dar es Salaam.
Mhe. Wambura ameeleza
kuwa ni muhimu kwa wafanyakazi kujumuika kwa pamoja katika michezo ili
kuboresha afya na kuimarisha uhusiano
baina yao.
“Michezo ni kitu
kizuri kwani husaidia katika kuimarisha na kulinda afya zetu hivyo ni vyema kila
mmoja wetu kushiriki katika michezo ili kuwa nguvu ya kutekeleza majukumu yetu
ya kila siku” alisema Mhe. Wambura.
Vilevile alitoa
shukrani kwa wakuu wote wa mabenki kwa
ushirikiano wao wa kuwaleta pamoja
wafanyakazi wa benki ili kufahamiana na kuimarisha ushirikiano baina yao.
Kwa upande wake Meneja
Masoko wa Benki ya Barclays Bw. Aron Luhanga amesema kuwa dhumuni la mashindano
hayo ni kuendeleza mahusiano baina ya benki kwa kufahamiana na kuimarisha afya
na fikra zao.
“mashindano haya ni
kwa ajili ya kufahamiana na kuimarisha urafiki kwa wafanyakazi wa sekta ya
benki kwa kufanya sekta ya kibenki kuwa sehemu bora ya shughuli za kiuchumi
nchini” alisema Bw.Luhanga.
Mashindano hayo ya
Brazuka kibenki yanaratibiwa na benki ya Barclays na ni mara ya pili kufanyika nchini
ambapo mwaka jana benki ya Diamond Trust (DTB) iliibuka mshindi hivyo kushiriki
katika ufunguzi wa michuano hiyo mwaka
huu.
Benki zinazoshiriki
mashindano hayo ni 18 ikiwemo Benki Kuu
ya Tanzania, NMB, Stanbic, KCB, Exim, Citi Benki, Commrcial Bank of Africa
(BOA),CRDB, Letshego, Eco Bwnki, Akiba, Diamond Trust Benki, Bank of India, Banc
ABC,Azania na Twiga Bancorp.






No comments:
Post a Comment