Mashabiki wa timu ya TP Mazembe wakishangilia timu yao ilipopambana na Yanga ya Tanzania katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana na Yanga kukubali kipigo cha bao 1-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wa Yanga wakiwadhihaki watani wao wa jadi, Simba, wakati wa mchezo dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Taifa, ambao watazamaji waliingia bure bila kulipa viingilio. Yanga kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa TP Mazembe.
Makocha wa Yanga, Hans Plujm (kulia) na wa TP Mazembe (kushoto), wakizungumza jambo walipokutana na kusalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya timu zao jana, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), wakipasha kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Yanga ya Tanzania jana.
Wachezaji wa Yanga wakipasha kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamejipaka rangi za timu yao hiyo, huku wakicheza ngoma kwa ajili ya kuishangilia timu yao hiyo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.
Mmoja wa shabiki wa Yanga, akiwa amevaa mawani kubwa akifuatilia matukio yaliyokuwa yakifanyika uwanjani hapo kabla ya kuanza kwa mchezo huo,
Wachezaji wa TP Mazembe (kushoto) na wa Yanga (kulia), wakiingia uwanjani tayari kuanza mpambano huo jana.
Wachezaji wa TP Mazembe na wa Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mpambano huo jana.
Wachezaji wa TP Mazembe wakipiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu kabla ya kuanza kwa mpambano huo jana.
Wachezaji wa Yanga wakipiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu kabla ya kuanza kwa mpambano huo jana.
Wachezaji wa TP Mazembe wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mpambano huo jana.
Benchi la ufundi la TP Mazembe likiongozwa na Kocha Mkuu
Salum Telela wa Yanga akikimbia na mpira huku akifuatwa na Adama Traore wa TP Mazembe.
Hapa ilikuwa ni heka heka kwenye lango la TP Mazembe wakati wa mpira wa kona uliolekezwa kwenye lango la timu hiyo katika mchezo huo.
Haruna Niyonzima wa Yanga akimtoka Nathan Sinkala wa TP Mazembe.
Christian Nikadio wa TP Mazembe akiudhibiti mpira uliokuwa ukiwania na Donald Ngoma wa Yanga.
Adama Traore wa TP Mazembe, akimtoka Juma Abdul wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Adama Traore wa TP Mazembe, akipiga mpira huku akifuatwa na Juma Abdul wa Yanga katika mchezo huo.
Mashabiki wa TP Mazembe wakishangilia bao pekee katika mchezo huo, lililofungwa na Mervelle Bope wa timu hiyo.
Ubao wa matokeo ukionesha Yanga 0 na TP Mazembe 1 mpaka mwisho wa mchezo huo.
Juma Abdul wa Yanga akikokota mpira huku akifuatwa na Issama Mpeko wa TP Mazembe.
Donald Ngoma (katikati) wa Yanga, akidhibitiwa na Christian Nikadio (kushoto) na Issama Mpeko wote wa TP Mazembe.
No comments:
Post a Comment