Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ally Samaje akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Tathmini ya maonesho ya tano ya kimataifa ya madini ya vito yaliyofanyika Jijini Arusha mwezi April mwaka huu yaliyo hudhuriwa na washiriki 813 kutoka nchi 26 duniani. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bi. Asteria Muhozya. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ally Samaje akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Tathmini ya maonesho ya tano ya kimataifa ya madini ya vito yaliyofanyika Jijini Arusha mwezi April mwaka huu yaliyohudhuriwa na washiriki 813 kutoka nchi 26 duniani. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bi. Asteria Muhozya.
WIZARA ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa madini
Tanzania (TAMIDA) iliendesha Maonesho ya tano ya Kimataifa ya Madini ya Vito
yaliyofanyika Jijini Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 19 hadi
21 Aprili, 2016. Maonesho haya hufanyika
kila mwaka Jijini Arusha na hukutanisha washiriki
mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wachimbaji, Wafanyabiashara wa madini ya vito wa
ndani na nje, wanunuzi wa madini wa
ndani na nje, na wataalam mbalimbali wenye uzoefu wa shughuli za madini ya vito.
Maonesho
hayo yalihudhuriwa na washiriki 813 kutoka katika nchi 26 duniani ambazo ni
Tanzania Marekani, Sri Lanka, India,
Kenya, China, Ujerumani, Namibia, Australia, Austria, Israel, Italia,
Uingereza, Hong Kong, Switzerland, Zambia, Madagascar, Afrika Kusini, Msumbiji,
Urusi, Cameruni, Canada, Malawi, Sudani, Malta, na Thailand). Aidha, wanunuzi (buyers) wa madini walikuwa 353,
Walioshiriki kuonesha madini kwenye mabanda (Exhibitors)
300, na wageni mbalimbali 160.
Lengo
kubwa la Maonesho haya ni kama ifuatavyo: kufanya Arusha kuwa kitovu cha madini
ya vito katika Afrika ili hatimaye iwe ni kitovu cha biashara ya madini hayo;
fursa ya masoko kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa mdini ya vito nchini; na
kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito hapa nchini.
Katika
maonesho hayo, madini yenye thamani ya Dola
za Marekani milioni 4.5, sawa na Shilingi
Bilioni 9.9 yaliuzwa.
Serikali
ilipata jumla ya Shilingi bilioni 1.71,
ambapo Shilingi bilioni 1.3
zilitokana na mnada wa madini yaliyokamatwa na kutaifishwa na Serikali, Shilingi milioni 388 zilitokana na
mrabaha uliolipwa kutokana na madini yaliyonunuliwa, na Shilingi milioni 26 zilitokana na vibali vya kusafirisha madini nje
ya nchi.
Manufaa
mengine yaliyopatikana wakati wa maonesho ni pamoja na wageni kuingiza fedha za
kigeni hapa nchini ambazo hutumika kwa ajili ya malazi, usafiri, chakula na
kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii hapa nchini.
Ili
kuweka utaratibu utakaodhibiti shughuli za madini ya vito hususani tanzanite, Serikali inakusudia
kuanzisha minada ya ndani mbali na mnada unaofanyika wakati wa Maonesho ya
Kimataifa ya Vito Jijini Arusha. Minada hiyo itatoa fursa kwa wafanyabishara wa
ndani kununua madini kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuongeza thamani madini hayo na kutengeneza vidani mbalimbali.
Ili
kuimarisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito nchini, Serikali inakusudia
kuimarisha Kituo cha Jimolojia kilichoko Arusha (Tanzania Gemmological Centre -TGC) ili kufundisha na kuzalisha
vijana wa Kitanzania wa kutosha wenye ujuzi wa kusanifu na kung’arisha madini
ya vito. Tayari vijana 29 wameshapata mafunzo ya miezi 6 ya ukataji wa madini
ya vito kutoka kwenye kituo hicho tangu 2014. Wanafunzi wengine 18 wanaendelea
na mafunzo ya miezi 6 yaliyoanza mwezi Machi, 2016.
Aidha,
upo mpango wa kuanzisha EPZ eneo la Merelani ambapo ni karibu na machimbo ya tanzanite
kwa lengo la kupata eneo maalum ambapo shughuli za biashara ya madini na uongezaji
thamani madini ya tanzanite zitafanyika kwa uhuru na wazi. Pamoja na juhudi
zote hizo, Serikali itaendelea kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa madini
mbalimbali nje ya nchi ikiwemo Tanzanite kwenye viwanja vya ndege na kwenye migodi
ambapo madini yanazalishwa.
Wito
wa Serikali ni kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini
kuzingatia sheria zilizopo wakati wa kufanya shughuli zao.
Imetolewa
na;
KAIMU KAMISHNA WA MADINI
MHANDISI ALLY SAMAJE
No comments:
Post a Comment