KAMA ningeweza kukutana Rais wa
Shirikisho la Soka nchini ningemshauri namna
bora ya kuanzisha vituo vya kukuza wachezaji chipukizi mikoa mbalimbali hapa
nchini kwani hiyo ndio itakuwa njia sahihi ya kuinua soka la Tanzania ili kutoa
fursa kwa wachezaji wa kitanzania kuweza kuchezea timu kubwa
duniani.
Kwa sababu hakuna mamna ya kuweza
kufanya ili tuweze kupiga hatua kubwa za
kimaendeleo ya mpira kwani bila kufanya hivyo kila siku tutakuwa tunapoteza
muda ambao una thamani kubwa kama ungeweza kutumiwa vizuri.
Hayo sio maneno yangu bali ni ya
mlinda mlango wa Kitanzania aliyewahi kufanya majaribio kwenye klabu ya
Chelsea ya nchini Uingereza Abbas Pira “Barthez”wakati akizungumza na mwandishi
wa makala hii ambapo anasema kwenye mafanikio ya soka hakuna njia za mkato
lazima kuwepo kwa dhamira ya dhati ya kupewa msukumo jambo
hilo.
Abas Pira ambaye aliwahi pia
kuichezea timu ya Coastal Union miaka ya nyuma
ilipokuwa ikishiriki Ligi Daraja la kwanza anasema ili Tanzania waweze kupata
mafanikio lazima kuanza na vituo vya kukuza soka kama ilivyokuwa nchi nyengine
duniani kwani hiyo ndio itakuwa dira na mabadiliko yatakayokuwa chachu ya
kufikia ndoto za kuchukua kombe la dunia siku moja.
Anasema umuhimu wa vituo hivyo
ndio utakuwa dira ya kulipeleka soka la
Tanzania kwenye hatua kubwa kwa sababu wataweza kupata wachezaji wengi wazuri
ambao wanaweza kuwa hazina kubwa kwa Taifa kwa kuzitumikia timu za Taifa kuliko
ilivyokuwa sasa.
“Unajua hata ukiangalia
kwenye nchi za nje zinapata mafanikio makubwa
kwenye soka kwa sababu ya kuwekeza kupitia timu za vijana na kufungua vituo vya
soka hivyo jambo hilo kama likitiliwa mkazo hapa kwetu tutafika mbali
“Anasema.
Aidha alisema ukiangalia kwa
Tanzania vituo vingi vya kukuzia soka
limejengwa kwenye baadhi ya mikoa michache na kuiacha mikoa yenye wachezaji
wenye uwezo na vipaji kushindwa kupata fursa hiyo adhimu kwa ajili ya maendeleo
yao.
Sambamba hilo lakini pia analitaka
shirikisho hilo kuweka utaratibu mzuri wa
kuunda kamati ya mawakala ambao watakuwa na kazi ya kuwachagua wachezaji ambao
wanaweza kuwapeleka kwenye kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ikiwemo kuweka
ufuatiliaji.
“Unajua suala la kuundwa
kamati ya mawakala ambao kila mwaka wanaweza
kuwa na orodha ya wachezaji wangapi wamekwenda kufanya majaribio nje ya nchi na
nafasi zao zipoje kwenye nchi ambazo wamekwenda kucheza
“Anasema.
Pirra ni nani na alitokea wapi kabla ya kwenda
Chelsea kwenye majaribio?
Abasi Pira anaanza kusema alianza kucheza mpira
katika timu ya Mzambarauni mwaka 1994 iliyokuwa na maskani yake jijini
Tanga baada
ya hapo alionekana na Kocha Joseph Lazaro ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya
Mgambo Shooting na kumpeleka timu ya
Coastal Union ambapo alicheza mechi za timu hiyo wakiwemo Juma Mgunda,Mohamed
Kampira,Saidi Mhando,Nyendi Mpangala ,Mwarami Saidi Deo Masanja na
Sande Peter.
Hao
ndio baadhi ya wachezaji ambao nina wakumbuka
tulikuwa pamoja wakati nikicheza kwenye timu ya Coastal Union ambapo nilidumu
kwenye timu hiyo mpaka mwaka 2005 wakati timu hiyo ilipokuwa ikishiriki Ligi
daraja la kwanza.
Mlinda mlango huyo ambaye alisoma kwenye shule ya
sekondari Popatlaly iliyopo Jijini Tanga kuanzia mwaka 2002 mpaka 2005 alianza
kung’ara kwenye medani ya soka hapa nchinio baada ya kuwa mchezaji bora kwenye
mashindano ya Umisseta.
Nini kilimpeleka nchini Uingereza?
Abasi anasema kuwa baada ya kumalizika kidato cha
nne katika shule ya sekondari Popatlaly alipata nafasi ya masomo kusomea nchini
Uingereza na hivyo kujikuta akilazimika kucheza mpira mtaani wakati anapokuwa
ametoka shuleni .
Anasema alicheza mpira kwenye timu za mtaani kwa
kipindi kirefu baadae watu walimuona na kumshauri kuongeza jitihada za kwenda
kucheza kwenye timu kubwa na ndipo alipokwenda kufanya majaribio kwenye klabu
za Chelsea kwenye dimba la Stanforde Brige na Klabu ya Birmingham
City
Kwanini
alishindwa kuchezea klabu ya Chelsea kama ilivyokuwa mipango
yake?
Mlinda mlango huyo anasema kuwa licha ya kufanikiwa
kucheza vema na kuvutia watu wengi kutokana na aina ya udakaji wake anapokuwa
langoni lakini kilichomnyima nafasi ya kupata namba kwenye timu hiyo ni
kutokana na kutouwa na rekodi ya kuichezea timu ya Taifa ya
Tanzania.
“Kutokuwa na
rekodi hii kumenifanya nishinde kupata namba ya kucheza Chelsea lakini pia
kitendo cha nchi yetu ya Tanzania kushindwa kuwepo kwenye nafasi ya 70 B or
kififa hilo ndio lilinikwaza kushindwa kupata kibali cha kucheza soka huko
“Anasema.
Anasisitiza kuwa sababu kubwa ndio hivyo kwani
hawajawahi kuichezea timu ya Taifa lakini pia kitendo cha Tanzania kutokuwepo
kwenye renki za juu kwenye shirikisho la soka dunia ilikuwa ni kikwazo kikubwa
cha yeye kufikia malengo yake.
“Lakini
pamoja na kupitia huku nimeenda pia kufanya majaribio kwenye vituo vya soka vya
CV Academy ya North Ontony ya England na sasa nimerudi nyumbani Tanzania lakini
pia nimesomea masuala ya Ukocha ngazi ya cheti kubwa zaidi nataka kuona kama
ninaweza kupata nafasi ya kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa
Stars”.
Lakini kabla ya kufikia hatua ya kuchezea timu ya
Taifa ya Tanzania hivi sasa anaangali namna yua kupata timu ambayo anawezea ili
aweze kuonekana na baadae apata fursa ya kuitumikia timu hiyo kwani kwa sasa
anafanya mazoezi kwenye timu za vijana za Boraska na Veteran kwa ajili ya
kujiweka imara.
Nini malengo yake katika soka?
Pira anasema kwanza lengo lake kubwa ni kuhakikisha
anapata namba ya kudumu kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ikiwemo kucheza kwenye
timu yoyote hapa nchini ikiwemo Yanga,Simba na Azam FC ili kuweza kuonyesha
uwezo wake aliokuwa nao.
Lakini pia anasema anaangalia namna ya kutafuta timu
nje ya nchi ili kuweza kuendeleza kipaji chake kwani bila kucheza soka kinaweza
kupotea na kutokuonekana kwake.
Anadhani watanzania wanakosea wapi kwenye
soka?
Anasema kuwa Tanzania inashindwa kufanya vizuri
kwenye medani ya soka kutokana na kutokuwepo kwa vituo vya kukuzia soka hasa
maeneo ya mikoani kwani vingi vimekuwa vikijengwa mkoani Dar es Salaam wakati
vipaji vingi vinatokea nje ya mkoa huo.
Sambamba na hilo pia akawageukia wachezaji
wanaosajiliwa na vilabu na timu za Taifa za Tanzania kuhakikisha wanatimiza
ndoto za wapenzi na mashabiki kwa kuvisaidia ili viweze kufikia malengo yake
kwani kutokufanya hivyo watakuwa hawana msaada.
“Lakini
nisema pia aliyeweza kuliweka soka la Tanzania kwenye ramani ni Maxio Maxime
ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa kwa sababu ujio wake hapa nchini
uliweza kubadilisha mfumo wa soka na sasa tunahitaji kupambana zaidi
“Anasema.
Historia ya mlinda mlango Pirra ambaye alizaliwa
February 20 mwaka 1988 alianza kuichezea timu ya Coastal Union akiwa na miaka
10 ambapo rasmi ilikuwa ni mwaka 1998 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2005 kabla ya
kwenda nchini Uingereza kimasomo.
Klabu ambazo aliwahi kuzifanyia majaribio ni Chelsea
mwaka 2010, Birmingham City Football Club,Colchesterter United mwaka 2011 na
mwaka 2012 alikwenda kufanya kujaribu pia bahati yake kwenye klabu ya MK Dons
lakini pia aliwahi kuchezea klabu ya Legton Oriet FC.
Anataka kufikia wapi kisoka “
Pirra anasema kuwa malengo yake makubwa ni kuwa kama
mlinda mlango Oliver Khan wa timu ya Ujerumani na Fabian Barthezi wa nchini
Ufaransa aliyeisaidia timu ya nchi hiyo kuchukua Ubingwa mwaka
1998.
MWISHO
MAKALA HII IMETAYARISHWA KWA HISANI YA TANGARAHABLOG
No comments:
Post a Comment