Wachezaji wa kikosi cha timu ya Al Ahly ya Misri wakipiga picha ya pamoja kabla ya mchezo wao wa kwa wa Ligi ya Mabingwa barani dhidi ya Yanga ya Tanzania, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Timu hizo zimefungana bao 1-1.
Wachezaji wa kikosi cha timu ya Yanga ya Tanzania, wakipiga picha ya pamoja kabla ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Donald Ngoma wa Yanga (katikati), akizuiya mpira kwa kichwa huku akikimbia nao kuwatoka wachezaji wa Al Ahly ya Misri.
Mashabiki wa timu ya Al Ahly, wakiwa wamevua fulana zao kuishangilia timu yao hiyo dhidi ya Yanga ya Tanzania wakati wa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa timu ya Al Ahly, wakiripua fataki baada ya timu yao kufanikiwa kupata bao kwenye mchezo huo.
Kocha wa Yanga, Hans Plujm, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Yanga, wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo, dhidi ya Al Ahly ya Misri, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment