TANGAZO


Monday, April 11, 2016

Watumishi hewa wamponza mkuu wa mkoa Tanzania

Magufuli

Image copyrightStatehouse Tanzania
Image captionRais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa wafanye uchunguzi kuwatambua watumishi hewa
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa.
Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.
Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza.
Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa kazini mara moja.
Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani.

No comments:

Post a Comment