TANGAZO


Friday, April 1, 2016

SHIRIKA LA POSTA KUZINDUA POSTA NYUMBANI JUMANNE WIKI HII

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huuKushoto ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika, James Mahanga na kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, alipokuwa akizungumza kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu
Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Shirika la Posta, Wilfred Miigo (kulia) na Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa shirika hilo, Joseph Ngowi, wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Meneja Masoko, David George (kushoto), Meneja Huduma za Barua, Fadya Zam (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Shughuli za Kimataifa, Elia Madules, wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wapigapicha wakiwa kwenye mkutano huo, wakimsikiliza na kuchukua maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, wakati alipokuwa akizungumza nao jijini, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, wakati alipokuwa akizungumza nao jijini, Dar es Salaam leo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe.
Baadhi ya waandishi wa habari na Maofisa wa shirika hilo, wakiwa kwenye mkutano huo jijini, Dar es Salaam leo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe.
Baadhi ya waandishi wa habari na wapigapicha wakiwa kwenye mkutano huo, wakisikiliza na kuchukua maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, wakati alipokuwa akizungumza nao jijini, Dar es Salaam leo, akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu shirika hilo, kuanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery), kuanzia Jumane Aprili 5, mwaka huu. Kushoto ni Meneja Mkuu Rasilimali za shirika, James Mahanga na kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Biashara za Shirika, Janet Msofe.

KATIKA kuhakikisha kuwa Shirika la Posta Tanzania linashiriki na kuchangia kikamilifu jitihada za  Serikali ya Awamu ya Tano za kuleta maendeleo ya haraka kwa mwananchi na kuifanya nchi yetu kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Shirika kuanzia Jumanne litaanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani au ofisini kwa mtumiwa (home/office delivery).

Huduma hii inayojulikana kama “Posta Mlangoni”itaanzia katika baadhi ya kata za hapa jijini Dar es salaam, Arusha na Dodoma inaboresha ile iliyokuwako tangu enzi za ukoloni ya masanduku yaliyoko Ofisi za Posta  ambayo mtumiwa analazimika kufuata yeye mwenyewe barua, vifurushi,taarifa au bidhaa alizotumiwa kupitia Ofisi za Posta. Kwa hivi sasa yako masanduku 173,000 yaliyosimikwa katika Ofisi za Posta 172 zilizoko nchini.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais (TAMISEMI) tayari imeweka miundombinu hiyo katika kata 8 za jiji la Arusha, kata 8 za manispaa ya Dodoma na kata 32 kwajiji la Dar es Salaam.  Miundo mbinu hiyo ni mitaa kuwekewa nguzo zenye kuonyesha jina la mtaa, nyumba zilizopo kwenye mtaa huo kuwekewa nambari za kiposta.

Mara baada ya kuanzisha huduma hii Jumanne ijayo hapa Dar es Salaam, Arusha na Dodoma ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2015/2016, awamu ya pili itakayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2016/2017 itahusu mikoa ya Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mara, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Pwani, Manyara, Simiyu na Geita pamoja na Tanzania Visiwani (Unguja na Pemba). Awamu ya tatu itatekelezwa katika kipindi cha mwaka 2017/18 itakamilisha mikoa yote iliyobaki ambayo ni Iringa, Mbeya, Songwe, Kigoma, Singida, Rukwa, Ruvuma, Katavi na Njombe.

Huduma hii ni msukumo mpya wa ndani ya Shirika wa kuhakikisha kuwa yanakuweko mabadiliko katika uendeshaji na utoaji wa huduma za mawasiliano ya Posta nchini ili kukabiliana na kasi ya teknolojia, kukidhi mahitaji ya soko, kuboresha maisha ya wananchi na kuifanya Tanzania kuwa kinara wa huduma bora za mawasiliano  barani  Afrika.

Kupitia huduma hii yamefanyika mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji katika baadhi ya Ofisi ili kuhakikisha kuwa uchambuzi wa barua unafanyika kwa uhakika na haraka zaidi, anwani zinatambuliwa kwa urahisi na kuongeza kasi katika kusafirisha na kusambaza barua, nyaraka, vifurushi na bidhaa za wateja.

Aidha, katika kipindi hiki cha mpito ambapo hapo baadae ndani ya kipindi cha miaka mitatu Shirika litasambaza huduma ya “POSTA MLANGONI” nchi nzima, mfumo wa sasa wa anwani kupitia  masanduku ya barua umeboreshwa ambapo  wateja au wananchi wenye barua katika masanduku yao watakuwa wanatumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu (sms) ili kufuata barua zao hizo badala ya utaratibu wa sasa ambapo wanalazimika kusafiri kwenda Posta bila ya taarifa ya kuwepo au kutokuwepo na barua katika masanduku yao.

Huduma hii imeanzishwa sasa kutokana na jitihada mahususi za Serikali kuweka Miundombinu ya Anwani za Makazi na Postikodi kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) na wadau wengine.  Miundombinu hii ni pamoja na Barabara/Mtaa kupewa majina yanayosomeka kwenye nguzo zilizosimikwa pamoja na nyumba kupewa namba kwa utaratibu rahisi  wa anwani pamoja na postikodi.

Postikodi  au zip codekama inavyojulikana katika nchi nyingine duniani ndiyo  inayorahisisha kumfikia mteja mahali alipo.  Postikodi ni alama za kiposta zenye namba zilizochanganywa na herufi ili kutambua sehemu husika.  Namba hizo zimeundwa kitaalamu kurahisisha usambazaji wa barua ili mlengwa aweze kuipata barua yake.  Nchini Tanzania, alama hizo zipo katika mfumo wa namba pekee zenye tarakimu tano bila kuchanganya na herufi.

Kila Kata/Wadi katika nchi yetu imepewa Postikodi hiyo yenye tarakimu hizo tano zenye kuwakilisha kata husika, wilaya iliyomo, mkoa na kanda.  Tanzania bara imegawanywa katika kanda (6) za kipostikodi kuanzia 1-6, huku Zanzibar ikipewa (7).  Hivyo kila Mtanzania anaweza kutambuliwa makazi yake kwa kata  anayoishi, Barabara/Mtaa/Kijiji/Kitongoji na namba ya nyumba. Kwa hivi sasa Serikali imekamilisha kanzidata (database) ya mfumo mzima wa  anwani za makazi kwa nchi nzima na hivyo kuwezesha anwani hizo kutambulika hadi ngazi ya kata/wadi hatimaye kuwezesha kila mwananchi kuwa na anwani inayomtambulisha.  Anwani na Postikodi hizo ziko katika tovuti za Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) www.tcra.go.tz na Shirika la Posta Tanzania (TPC) www.posta.co.tz.

Shirika la Posta Tanzania linatambua na kuzingatia kuwa mifumo ya huduma za mawasiliano hususani haya ya Posta inabadilika kwa kasi sana duniani. Kwa mfano, baadhi ya nchi zilizoendelea ziko katika tafiti na majaribio ya mwishomwisho ya kuendesha huduma za Posta kwa kutumia mashini za roboti au ndege zisizokuwa na rubani (drones), mfano Singapore na Uswizi.

Kwahiyo, pamoja na malengo mengine muhimu, malengo halisi ya Shirika ya kuanzisha huduma ya “POSTA MLANGONI” ni kuhakikisha kuwa watanzania wanafaidika na matunda ya huduma bora na za kisasa za usambazaji na logistiki, huduma bora za kimtandao kama manunuzi mtandao (e – shopping) kitaifa na kimataifa, kuwaongezea kasi katika matumizi ya sayansi na teknolojia, kuwapunguzia umaskini na kwa ujumla kuwarahisishia uendeshaji wa maisha yao ya kila siku ya kiuchumi na kijamii.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA POSTAMASTA MKUU
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
POSTA HOUSE, GHOROFA YA 12
7 MTAA WA GHANA
11300 DAR ES SALAAM
SIMU:   022 21133 94
068 48875 61
068 48879 66

No comments:

Post a Comment