Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Posta wa TCRA Bw.Haruni Lemanya jinsi mitambo ya mawasiliano ya kizamani iliyowekwa katika makumbusho ya mawasiliano iliyopo katika ofisi za mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA). Kulia kwake ni ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk.Ally Simba akifatilia kwa karibu.
Naibu Mkurugenzi Idara ya Utangazaj i(TCRA), Bw. Frederick Ntobi akieleza jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye jinsi uangalizi wa maudhui ya Utangazaji yanavyofanyika na mamalaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk. Ally Simba na Meneja mawasiliano wa mamalaka hiyo Bw.Innocent Mungy(wa kwanza kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk. Ally Simba(katikati) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye jinsi kituo cha usimamizi wa mawasiliano kinavyofanya kazi katika mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dk. Ally Simba(wa kwanza kulia) na wajumbe wa kamati ya maudhui ambao ni mwenyekiti wa kamati hiyo margareth munyagi (wa tatu kushoto), Abdul Ngarawa (wa nne kulia), Joseph Mapunda (wa pili kulia), Zainabu Mwatawala (wa tatu kulia) na Derek Murusuri (wa pili kulia).
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewaasa wajumbe wa kamati ya
Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kujenga mazoea ya kuelimisha Umma
badala ya kusubiri makosa ili waweze kutoa adhabu.
Hayo, yamesemwa na
Waziri waHabari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Moses Nnauye alipokuwa akizindua
kamati hiyo ya Maudhui leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania.
Alisema nivyema kama wadau
wakuu wakafahamu majukumu ya kamati hiyo na kuelimishwa nini wanachopaswa kukifanya
ili kuzuia baadhi ya makosa ambayo yangeweza kuzuilika na kuongeza kuwa kingani
bora kuliko tiba.
Katika uzinduzi wa kamati
hiyo pia alitoa wito wa kuangalia jinsi ambavyo vyombo vya habari wanazingatia sheria
ya matumizi ya asilimia sitini ya maudhui ya Kitanzania katika vipindi vyao kwani
suala hilo bado linalalamikiwa na wadau wengi.
“Najua kuna ugumu wa kuisukuma
hiyo sheria, ila isimamiwe vizuri, takwimu hazifurahishi sana na kama inaonekana
sheria hiyo haitekelezeki ni bora iangaliwe kwa upya” alisema waziri.
Kwa upande wake mjumbe
wa kamati hiyo, Bw. Joseph Mapunda alisema kuwa licha ya umakini watakao kuwa nao
katika kutekeleza majukumu yao Kamati imedhamiria kuhakikisha inahamasisha suala
la mafunzo kwa watangazaji yanatiliwa mkazo kwani watangazaji wengi hawana mafunzo
bora yautangazaji.
Aliongeza kuwa asilimia
kubwa ya watangazaji nchini wanafanyakazi katika mazingira magumu inayopelekea utendaji
usio na tija, hivyo, kamati yao itafanya ushawishi kuhakikisha wanathaminiwa na
kufanyakazi katika mazingira rafiki.

No comments:
Post a Comment