Waziri wa Habari, Utamaduni, SanaanaMichezo Mhe. Nape Nnauye (wapili kushoto) akiwa na Mkuu wa Mafunzo na Operesheni Jeshi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Issa S. Nassoro (wa kwanza kushoto) wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Ngumi uliotelewa na Wizara hiyo kwa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ). Wengine pichani ni Brigedia Jenerali Martin Busungu ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo jeshini (wapili kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Alex Nkenyenge.
Waziri wa Habari, Utamaduni, SanaanaMichezo Mhe. Nape Nnauye akimvisha medali bondia wa jeshi kama moja ya ishara ya ufunguzi wa ulingo wa ngumi waliopewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuimarisha mchezo wa ngumi jeshini na nchini kwa ujumla kwani ulingo huo, utatumiwa na Baraza la Michezo ya Majeshi kujiimarisha katika mchezo huo. Wengine pichani ni Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa JWTZ Meja Jenerali Issa S. Nassoro (wa kwanza kushoto).
Waziri wa Habari, Utamaduni, SanaanaMichezo Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa JWTZ Meja Jenerali Issa S. Nassoro ulingo wa Ngumi wa kisasa ambao wizara ilipewa na Serikaliya China kwa ajili ya maendeleo ya ngumi nchini. Wizara imeamua kuwapa jeshi kwa kuwa ni sehemu salama na watakuwa na nidhamu ya kuutunza na pia ulingo huo utaimarisha Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA). Wengine pichani ni Brigedia Jenerali Martin Busungu ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo jeshini (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge (wa kwanza kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni, SanaanaMichezo Mhe. Nape Nnauye akipiga gitaa pamoja na bendi ya jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ)
wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Ngumi uliotelewa na wizara hiyo, kwa jeshi hilo leo, jijini
Dar es Salaam.
Picha zote na Daudi Manongi-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM).
No comments:
Post a Comment