Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (aliyesimama) akizungumza na wadau wa sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mhe. Nape Nnauye kukutana na wadau hao jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga na kulia ni katibu wa CCM Mwanza Ndg. Miraji Mtaturu.
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Ndg. Atley Kuni akitoa taarifa ya sekta ya habari kwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Mhe. Nape Nnauye kukutana na wadau wa sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo.
Msanii kutoka jiji la Mwanza Ndg. Feizal Saul (aliyesimama) akichangia wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji jana Jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi iPad afisa habari kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw. Stephen Msengi wakati wa ziara ya yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Meneja wa Star times kanda ya ziwa Bw. Bakari Hassani (kushoto) alipotembelea ofisi hizo wakati wa ziara yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watendaji wa TBC pamoja na Star Times nje ya ofisi za TBC zilizopo jijini Mwanza jana wakati wa ziara yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo. Wapili kushoto ni Meneja wa Star times kanda ya ziwa Bw. Bakari Hassani na watatu kulia ni Kaimu Mkuu wa Kanda ya ziwa TBC Bibi. Rachel Mwasha.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na viongozi wa CCM
Mkoa wa Mwanza alipowasili katika uwanja vya CCM Kirumba kupata taarifa ya
uwanja huo wakati wa ziara yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia
pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea
viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo Jijini Mwanza. Kushoto ni
Katibu wa CCM Mwanza Ndg. Miraj Mtaturu.(Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo, Mwanza)
No comments:
Post a Comment