Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema mwamuzi alifaa kuzingatia sifa za kiungo wa kati wa klabu hiyo Juan Mata kabla ya kumfukuza uwanjani.
United walicheza wachezaji 10 uwanjani dhidi ya West Brom kwa zaidi ya saa moja baada ya refa Mike Dean kumpa kadi ya pili ya njano mchezaji Juan Mata.
Walilazwa 1-0 kwenye mechi hiyo ya Ligi ya Premia uwanjani Hawthorns.
Mata hajawahi kufukuzwa uwanjani awali katika Ligi ya Premia lakini kwenye mechi hiyo ya Jumapili alionyesha kadi mbili za manjano katika kipindi cha dakika tatu.
"Refa anafaa kuzingatia sifa za mtu anayemvaa mpinzani na Mata hajawahi kumuumiza mchezaji,” amesema Van Gaal.
"Unaweza kumuonesha mtu kadi mbili za manjano kwa mujibu wa sheria lakini nafikiri refa anafaa kujua ni mchezaji yupi anayefanya hivyo,” aliongeza meneja huyo.
"Hii ndio maana refa mwenye uzoefu huwa bora sana kwa sababu anawafahamu wachezaji vyema, anaufahamu mchezo. Nafikiri unafaa kuzingatia hilo.”
Mechi hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa United kushindwa na West Brom uwanjani Hawthorns tangu 1984.
United kwa sasa wamo nambari sita ligini.
No comments:
Post a Comment