TANGAZO


Monday, March 7, 2016

Liverpool yapeta,Man U yachapwa

Image copyrightAP
Image captionWachezaji wa Liverpool
Ligi kuu ya England iliendelea tena mwisho wa wiki kwa michezo miwili kuchezwa.
Majogoo wa Anfield Liverpool wakicheza ugeni kwenye dimba la Selhurst Park waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace.
Crystal Palace ndio walianza kuandika bao la kwanza kwa bao la Joe Ledley kisha Liverpool wakachomoa bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wake Roberto Frimino, katika dakika za lala salama Christian Benteke akawapa ushindi kwa bao la mkwaju wa penati.
Nao Mashetani Wekundu wa Man United wakachapwa kwa bao 1-0 na West Bromwich Albion, bao hilo pekee likifungwa na Solomon Rondon, huku kiungo wa Juan Mata akitolewa nje kwa kadi nyekundu.

No comments:

Post a Comment