Mkurugenzi wa Kituo cha Yatima na wale waliotoka katika mazingira magumu cha Watoto Wetu Tanzania (WWT), Evans Tegete akizungumza na wanahabari mwishoni mwa wiki wakati akipokea misaada mbalimbali kutoka Shule ya Awali ya Sunrise.
Mwalimu wa Shule hiyo, Suma Mwasuka (katikati), akizungumza na wanahabari.
Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Anne Nyokabi (mbele), akiongoza wenzake kufanya usafi Coco Beach ikiwa ni kuunga mkono kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Shughuli za usafi zikiendelea.
Uhamasishaji wa usafi ukiendelea.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wamekaa na wenzao wa Kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania walipofika kuwajulia hali na kuwapa misaada mbalimbali iliyolewa na wazazi, walimu na mwanafunzi mmoja mmoja.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wamekaa na wenzao wa Kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania walipofika kuwajulia hali na kuwapa misaada mbalimbali iliyolewa na wazazi, walimu na mwanafunzi mmoja mmoja.
Mkuu wa Shule ya Sunrise, Vitalis Onesphor (kulia), akizungumza na wanafunzi hao.
Walimu wa Shule ya Sunrise wakiwa kwenye hafla hiyo ya kutoa msaada kwa watoto hao.
Mkuu wa Taaluma (Brook house, Omega Ibrahim (kulia), akizungumza na watoto hao huku akiwapa neno la mungu kuhusu upendo.
Misaada ikitolewa.
Misaada ikikabidhiwa kwa wanafunzi wa kituo hicho.
Vitu mbalimbali vilivyotolewa kwa watoto wa kituo hicho.
Wanafunzi wa Sjule hiyo ya Awali ya Sunrise wakitoa misaada kwa watoto wenzao wa kituo hicho.
Na Dotto Mwaibale
UONGOZI wa Kituo cha kulelea Yatima na watoto waliokolewa katika mazingira magumu cha Watoto Wetu Tanzania (WWT) cha Kimara jijini Dar es Salaam, wameiomba jamii kuelekeza macho katika kusaidia vituo kama hicho ili kuvipa uwezo wa kulea watoto na kupunguza watoto wanaoteseka mitaani kwa kukosa msaada.
Katika hatua nyingine kituo hicho kimeiomba serikali kujipanga upya kusaidia vituo vya yatima ili kuondokana na mfumo wa sasa wa kusaidia pindi inapojisikia hivyo kusababisha idadi ya watoto na wahitaji wengine kuongezeka.
Hayo yalibainishwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa kituo hicho, Evans Tegete wakati akipokea msaada wa vyakula, sabuni na nguo kutoka kwa wanafunzi, wazazi na uongozi wa shule ya Awali na Msingi Sunrise vyenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 3.
"Msaada huu tuliopokea leo umefika wakati muafaka tuansema asante ingawa changamoto kubwa ni mahitaji tuliyonayo ni mengi na hayalingani na msaada tunaopata" alisema Tegete. tunashukuru, lakini lazima.
Tegete alisema kituo hicho hakina mfadhili wa kudumu mbali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front ambao mara kwa mara viongozi na waumini wake wamekuwa wakijitoa na kufika kuwasaidia kila wanapopata chochote.
Alisema kwa sasa kituo chake kina watoto 108 na 48 kati yao wanasoma katika ngazi mbalimbali ya elimu kuanzia msingi hadi vyuo vikuu ingawa wanafunzi 11 wameshindwa kuanza kidato cha kwanza kwa sababu kituo hakijawalipia ada ya sh.milioni 1.1 kila mmoja licha ya kupunguziwa ada kutoka sh.milioni 1.8 ya kawaida.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Shule ya Sunrise ya Jijini Dar es Salaam, Vitalis Onesphor, alisema msaada waliokabidhi kwa watoto wa kituo hicho umetokana na michango ya uongozi wa shule, wanafunzi na wazazi wenye watoto wanaosoma shuleni hapo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo kituo hicho, Issack Shomari alisema wamepokea msaada huo kwa mikono miwili kwa sababu umewafikia katika kipindi muafaka cha sikukuu ya Pasaka.
Shule hiyo Sunrise pamoja na kutoa msaada huo pia walifanya shughuli ya usafi Coco Beach pamoja na kupanda miti. (Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment