TANGAZO


Wednesday, March 30, 2016

Sanlam Life Insurance Tanzania Yazindua Bima ya Elimu

Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe na kulia ni Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (wapili kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Elimu ya 'Sanlam Education Care', Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava na kulia ni Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Elimu ya 'Sanlam Education Care', Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava na kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Elimu ya 'Sanlam Education Care', Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (wapili kushoto), akimkabidhi mkataba wa Bima ya Elimu wa 'Sanlam Education Care', Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando na kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (wapili kushoto), akimkabidhi mkataba wa Bima ya Elimu wa 'Sanlam Education Care', Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando na kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (wapili kushoto), Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando (kulia) na Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood (kushoto), wakinukuu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, jijini leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano wa uzinduzi huo, wa Bima ya Elimu ya 'Sanlam Education Care', Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe, akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, Dar es Salaam leo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (katikati), akifafanua jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa bima hiyo ya Elimu. Kulia ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava na kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood.
Maofisa wa Kampuni ya Bima ya Sanlam, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Bima ya Elimu wa 'Sanlam Education Care', leo jijini Dar es Salaam. 
Maofisa wa Kampuni ya EGT na wa Kampuni ya Bima ya Sanlam, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo, leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa EGT, Imani Kajula na wapili ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha wa kampuni ya Sanlam, Wilson Mnzava.

Dar es Salaam, 3 Machi 2016: 
KAMPUNI inayoongoza kwa utoaji wa bima za maisha Tanzania Sanlam Life Insurance, leo, imezindua bima ya elimu ya kipekee inayolenga kukupa uhakika wa elimu ya mwanao.

'Bima hiyo inayoitwa “Sanlam Education Care', inawapa wazazi mpango wa akiba wa kila mwezi pamoja na faida ya bima ya maisha ambayo inalinda uwekezaji wako katika tukio la kifo au ulemavu wa kudumu. 

Julius Magabe , Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, anasema,"kuwekeza katika elimu ya mtoto wako ni moja ya zawadi bora ambayo wazazi wanaweza kuwapatia watoto wao”. Elimu imeanza kuwa huduma ghali katika maisha ya siku hizi, kwahiyo wazazi wanashauriwa kufanya maamuzi ya busara ya uwekezaji pale linapokuja suala la ustawi wa maisha ya baadaye ya watoto wao. 

Sanlam Education Care ni suluhisho kamili, kwani imebuniwa kama mpango wa akiba unaowawezesha wazazi kuwa na utaratibu mahususi wa kuweka akiba ambao unazingatia kupanda kwa gharama za elimu.

"Hakuna huduma nyingine ya bima ya maisha inayokidhi haja ya kulinda elimu ya mtoto kama 
huduma hii ya Sanlam Education Care. ‘Kuongezeka kwa huduma ya Sanlam Education Care kwenye
orodha ya bidhaa zetu' inatilia mkazo dhamira yetu ya kupanua wigo wa huduma zenye ubunifu na 
zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu  pamoja na kuboresha na kulinda ukwasi wao", alihitimisha 
Bw. Magabe.

No comments:

Post a Comment