Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (wa pili Kushoto) akionesha kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi katika uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dare s Salaam Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Johavanes Aikaeli wa pili kulia ni Prof Lician Msambichaka Mhariri Mkuu wa kitabu hicho na kulia ni Prof. Delphin Rwegasira kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (wa pili kulia) akionesha kitabu pamoja na Mhariri Mkuu wa kitabu hicho kwa washiriki na waandishi wa habari Prof Lician Msambichaka katika uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Johavanes Aikaeli na kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sayansi na Jamii (UDSM) Prof Godius Kahyarara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akielezea mambo muhimu aliyoyaona katika kitabu alichokizindua kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Johavanes Aikaeli.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akielezea jambo kwa washiriki na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi.
Baadhi ya washiriki toka Idara ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (hayupo pichani) wakati kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki toka Idara ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (hayupo pichani) wakati kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa uchumi kutoka Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam mara baada ya kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Na Raymond Mushumbusi ,MAELEZO
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi
amezindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika
umasikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Dkt Abdallah Possi amesema amefurahishwa sana kuona wasomi wa Tanzania
wakijitolea muda wao na nguvu zao kushirikiana na Serikali katika kuondokana na
umasikini ili tuelekee katika ustawi wa taifa.
“ Kitabu hiki kimekuja wakati muafaka
ambapo Serikali ya awamu ya tano imejikita katika mapinduzi na maendeleo katika
sekta ya viwanda ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi
nyingi duniani kwa sasa, hivyo tunaahidi kushirikiana na watafiti mbalimbali
katika kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazotukabili katika kuondokana na
umasikini,”Alisema Dkt. Possi.
“ Nimekisoma hiki kitabu kwa ufupi na
kuonda ni jinsi gani kitaweza kutusaidia katika mapambano dhidi ya umasikini
lakini napenda kuwapa changamoto kuwa kazi hii ya kupambana na umasikini isiwe
katika vitabu tu na sera bali iwe katika utekelezaji” Aliongeza Dkt Possi.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa
watafiti wa mambo ya uchumi wanatakiwa kuwashirikisha pia watu wenye ulemavu
katika harakati za kuondokana na umasikini kwa kuwashirikisha katika uundwaji
wa sera na utekelezaji wake katika kuleta maendeleo ya taifa.
Aidha Mhariri mkuu wa kitabu hicho,
Prof Lucian Msambichaka amesema dhima kubwa ya kitabu hicho ni utekelzaji wa
Sera,Mipango, Sheria na majukumu mbalimbali yahusuyo maendeleo kwa taifa na
kuongeza kuwa kitabu hicho pia kimetoa njia bora na muafaka wa kukuza sekta ya
viwanda, kuboresha huduma za jamii, kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na
jinsi gani Tanzania inavyoweza kunufaika na maliasilia zake katika kujileta
maendeleo.
Kitabu hiki kimeandaliwa na Idara ya
Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kudhaminiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kimeshirikisha waandishi zaidi ya 20 na kina kurasa zaidi ya 400 ambazo
zimeelezea kwa kina namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kuondokana na umasikini na
kuelekea katika ustawi.

No comments:
Post a Comment