Ibrahim Ajib akipongezwa na wachezaji wenzake
IKIWA ni tunzo ya 4 tangu kuanza kwa zoezi la
kumchagua mchezaji bora wa mwezi ambapo zoezi hili lilianzishwa mwezi Septemba,
2015 likiwa na dhumuni la kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya
vizuri.
Mshambuliaji Ibrahim Ajibu ameshinda kwa mara ya
pili tunzo ya mchezaji bora mwezi Januari, 2016 baada ya kupigiwa kura kwa
wingi na wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba na soka la Tanzania kwa
ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News
pamoja na kwenye mitandao rasmi ya kijamii ya Simba Facebook www.facebook.com/simbatanzania
Twitter na Instagram @simbasctanzania.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Rais wa
Simba Evans Aveva alisema “sisi kama uongozi wa klabu yetu ya Simba tunaamini
katika kuwapa motisha wachezaji wetu kila iitwapo leo na hii ni katika kuongeza
chachu ya maendeleo si tu kwa mchezaji bali kwa klabu nzima kwa ujumla, Ajib
anashinda tunzo hii kwa mara ya pili mfululizo. Wote mtakubaliana nami kuwa kwa
kiwango anachoonesha mshambuliaji Ajib ni kweli mshabiki, wanachama na wapenzi
wa Simba hawajakosea kumchagua tena mshambuliaji wetu huyu.”
Napenda kutoa wito kwa wachezaji wetu wote
kuendelea kujituma zaidi kwani mashabiki wao wakiongoza na uongozi mzima
tunamatumaini makubwa msimu huu 2015/2016, tukiamini kwenye falsafa yetu ya
SIMBA NGUVU MOJA, aliongeza Rais Evans Aveva.
Akizungumza na simbasports.co.tz Mkurugenzi Mkuu
wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba,
Imani Kajula alisema “EAG Group inapenda kusisitiza kuendelea kuongeza utayari
wake katika kushirikiana na klabu ya Simba kwenye kutoa motisha kwa wachezaji
wa Simba ambapo italeta chachu ya kufanya vizuri zaidi na hivyo kuweza
kutengeneza mfumo mzuri wa kuongeza vyanzo vya mapato na hatimaye faidi kubwa kwa
wachezaji na timu kwa ujumla”.
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili
kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo
matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za
klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 kisha
utaletewa ujumbe jibu kwa kutuma neno “OK” na hapo utakuwa umejiunga rasmi,
Huduma hii ni maalum kwa Tigo na Vodacom.


No comments:
Post a Comment