Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akielezea jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin na kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akifurahia jambo alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution ambao ni wadhamini na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin, Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa na Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle NA Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akikabidhiwa zawadi kutoka TBL kwa makini
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) kupitia Bia yake ya
Kilimanjaro Lageralipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Kutoka
kushoto Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka
kulia) na Meneja Masuala ya Nje na Mawasiliano Bibi. Emma Oriyo.
12/02/2016
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika mashindano ya Kilimanjaro Marathoni yatakayofanyika tarehe
28 Februari kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Hayo
yamebainisha na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution ambayo ndio
waratibu wa mbio hizo Bw. Aggrey Marealle walipotembelea ofisini kwa Waziri leo
jijini Dar es Salaam.
“Mbio
za Kili Marathon zinatarajia kufanyika tarehe 28 mwezi huu katika viwanja vya
Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ambapo mgeni rasmi atakuwa Mhe. Nape Moses Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo”. Alisema Marealle.
Marealle
alisemakuwa Mbio hizo zitakuwa katika
makundi manne ambayo ni mbio za Kilomita 42 ambazo ndiyo marathoni yenyewe
inayothaminiwa na TBL kupitia bia ya Kilimanjaro,zingine ni Nusu Marathon za
kilomita 21 zinazodhaminiwa na Tigo,mbio za kilomita 10 zinazowashirikisha
walemavu wanaotumia Baiskeli za matairi matatu na Viti vya matairi
zinazodhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Gapco na mbio zinginge ni za kilomita 5
ambazo zinadhaminiwa na TBL kupitia kinywajji cha Grand Malt.
Aliongeza
katika mbio hizo washindi kumi kila kundi watapewa zawadi ambapo mshindi wa
kwanza kwa mwanaume na mwanamke katika mbio za kilomita 42 watapatiwa zawadi ya
shilingi milioni nne kila mmoja.
Aidha
alisema kuwa zaidi ya washiriki 7000 wanakadiriwa kushiriki mbio hizo huku kati
yao takribani washiriki 1000 watatoka nje ya nchi.
Kilimanjaro
Marathon inatimiza miaka 14 tokea kuanzishwa kwake ambapo waandaji wa
mashindano hayo ni Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini na kuratibiwa na
Executive Solutions Ltd ya Tanzania na mdhamini mkuu wa mbio hizo ni Kampuni ya
Bia TBL kupitia Bia ya Kilimanjaro Lager.







No comments:
Post a Comment