Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
wadau mbalimbali wa habari katika
kuadhimisha siku ya radio duniani
iliyoratibiwa na shirika la UNESCO leo
jijini Dar es Salaam.
Na
Lorietha Laurence-Maelezo
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel amewataka wamiliki wa radio
kuhakikisha kuwa wanafuata sheria,
kanuni na taratibu za uendeshaji pamoja
na kuandaa vipindi vyenye maudhui yanayoelimisha na kujenga jamii.
Aliyasema
hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari katika
maadhimisho ya siku ya radio yaliyoratibiwa na shirika la UNESCO katika kutambua
umuhimu wa radio za jamii.
“Ikiwa
wamiliki wa redio watazingatia kutoa
maudhui sahihi kwa jamii basi jamii husika itakuwa imejengwa katika msingi
ulioimara na dhabiti kwa ajili ya kuleta
maendeleo na maelewano,” alisema Prof. Gabriel.
Prof.Gabriel
aliongeza kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau katika kuhakikisha
kuwa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji zinazotolewa na Mamlaka ya
Mawasiliano Nchini (TCRA) zinafuatwa ili kuepuka msuguano baina ya wamiliki wa
radio na serikali.
Vilevile
alibainisha kuwa radio ni chombo muhimu sana kwa kuwa kinawafikia watu wengi kutokana
na kukua kwa teknolojia ambapo watu wanaweza kusikiliza radio popote wanapokuwa
kwa kutumia simu zao za mkononi, tofauti na vyombo vingine vya habari.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA)
Bi. Eda Sanga anaeleza kuwa kwa sasa
vipindi vingi vya radio vina maudhui
hafifu tofauti na zamani.
“Maudhui
ni kitu muhimu sana kwa kuwa kupitia maudhui watu wanapata taarifa na kuelimika
lakini zama hizi vipindi vingi vina maudhui ya muziki zaidi kuliko kuelimisha
umma” alisema Bi. Sanga.
Bi.Sanga
amewataka waandaji wa vipindi kujikita
zaidi katika kuandaa vipindi vyenye maudhui muhimu kwa kufanya utafiti wa kina
na kuangalia matokeo ya vipindi kwa jamii husika.

No comments:
Post a Comment