Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna.
Na Immaculate
Makilika- MAELEZO.
BAADHI ya Mawaziri na Manaibu Waziri wasiorudisha fomu
za Tamko la Rasilimali na Madeni na fomu
ya Ahadi ya Uadilifu wamesisitizwa
kurudisha fomu hizo leo kabla ya saa 12
jioni katika ya Ofisi ya Tume ya Maadili iliyopo jijini Dar es salaam na watakaoshindwa kufanya hivyo watakua
wamejitoa wenyewe kwenye nafasi zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majliwa ofisini kwake alipokutana na Waandishi
wa Habari akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki, ambapo ameeleza kuwa, kufuatia Semina iliyofanyika Februari 25 mwaka huu kati yake
na Mawaziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na
Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu, ambapo Kamishna Mkuu, Mhe. Jaji Mstaafu
Salome Kaganda alitoa maelezo kwamba kuna baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao
hawajarudisha fomu hizo hadi kufikia
jana.
Akiwataja Viongzoi hao, Mhe. Majaliwa alisema kuwa, Mawaziri
ambao hawajarudisha fomu hizo ni akiwemo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.
Charles Kitwanga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano,
Mhe. January Makamba, ambao wote hawajarudisha fomu za Rasilimali na Madeni na
fomu za Ahadi ya Uadilifu, vilevile Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine
Mahiga ambaye hajarudisha fomu ya Ahadi
ya Uadilifu, na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Profesa Joyce
Ndalichako, ambaye hajarudisha fomu ya Tamko
la Rasilimali na Madeni, pamoja na Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. Luhaga Mpina ambaye
hajarudisha fomu zote mbili.
Mhe. Majaliwa, amewasisitiza Mawaziri hao kujaza fomu hizo
kwa kua ni agizo la Mheshimwa Rais kujaza fomu hizo leo kabla ya saa 12 jioni, “viongozi
watakaoshindwa kutoa Tamko la Rasilimali
na Madeni na fomu ya Ahadi ya Uadilifu wanatakiwa
kujieleza kwa kutoa sababu za kushindwa kufanya hivyo na watachukuliwa hatua” alisema
Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 9 Sheria ya Maadili ya Uongozi wa
Umma ya mwaka 1995 sura ya 8 inawataka viongozi wote wa umma kujaza
fomu za kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma (Tamko la Raslimali na Madeni) na
fomu ya Ahadi ya Uadilifu mara wanapoteuliwa kushika nafasi mbalimbali za
uongozi. Lengo la kujaza fomu hizo ni kuwa na uwajibikaji kwa kiongozi juu ya
uadilifu wake wakati wote anapokua mtumishi wa Umma.
No comments:
Post a Comment