TANGAZO


Wednesday, February 3, 2016

Martinez wa A. Madrid ahamia China

Image copyrightEPA
Image captionMartinez wa A. Madrid ahamia China
Klabu ya soka cha Uchina , Guangzhou Evergrande, kimevunja rekodi ya nchi hiyo kwa kima cha fidia ya kumsajili mchezaji katika timu yao.
Klabu hiyo imelipa karibu dolla million 45 kusajili huduma za mshambuliaji wa kutoka Colombia , Jackson Martinez.
Martinez ambae sasa ameihama timu ya uhispania Atletico Madrid ametia sahihi kandarasi ya miaka minne.
Aliwahi kuifungia Atletico mabao 22 baada ya kuhamia Uhispania kutoka Porto.
Yeye ndiye mchezaji wa kiwango chake kuhamia Uchina baada ya kiungo cha kati wa Chelsea Ramires kuhamia Jiangsu Suning.
Si hao tu pia kuna Gervinho na Fredy Guarin waliohamia hukohuko China.
Kwa kutumia kitita kikubwa namna hiyo sasa ligi kuu ya Uchina inaikurubia ligi ya Uingereza kwa kima cha fedha zinazotumuka katika kuendesha soka nchini humo.
Ununuzi na usajili huo wa wachezaji umeshika kasi katika vilabu vya Uchina baada ya matamshi ya hivi karibuni ya rais Xi Jinping, ambae mwenyewe ni shabiki sugu, akisema kuandaa, kufuzu na kushinda kombe la dunia sasa ni miongoni mwa kipaumbele cha taifa hilo kubwa zaidi duniani.
Image copyrightBBC World Service
Image captionAliwahi kuifungia Atletico mabao 22 baada ya kuhamia Uhispania kutoka Porto.
Kocha wa Martinez huko Guangzhoualiwahi ifunza Chelsea na Brazil ,Luiz Felipe Scolari.
Akiwa huko atajiunga na kiungo cha kati wa zamani wa Tottenham Paulinho na Robinho .
Kwa mujibu wa takwimu za gharama ya uhamisho ligi hiyo ni ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment