Timu ya taifa ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imeshuka dimbani Amahoro kucheza dhidi ya Guinea mechi ya nusufainali.
DR Congo walifika nusufainali kwa kuwatoa wenyeji Rwanda.
Dakika ya 85 mambo bado ni 0-0.
Mchezaji wa DR Congo Padou Bompunga alipewa kadi ya njano dakika ya 38. Hili lina maana kwamba hataweza kucheza fainali iwapo timu yake itafuzu.
Kipa wa DR Congo Ley Matampi pia amepewa kadi ya njano, kosa lake likiwa kunawa mpira nje ya eneo lake.
Mechi hiyo imeanza saa kumi na moja alasiri saa za Afrika Mashariki.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ni miongoni mwa wageni mashuhuri wanaohudhuria mechi hiyo.
Nusufainali hiyo nyingine itachezwa kesho Alhamisi kati ya Ivory Coast na Mali.
- Ley Matampi
- Joyce Lomalisa
- Padou Bompunga
- Mechak Elia
- Doxa Gikanji
- Christian Ngudikama
- Nelson Munganga
- Merveille Bope
- Joel Kimwaki (Nahodha)
- Jonathan Bolingi Mpangi
- Yannick Bangala
- Abdoul Aziz Keita (nahodha)
- Mohamed Thiam
- Ibrahima Sory Bangoura
- Alseny Bangoura
- Ibrahim Sory Sankhon
- Ibrahima Sory Soumah
- Moussa Diawara
- Jean Mouste
- Alseny Camara
- Mohamed Youla
- Aboubacar Leo Camara
No comments:
Post a Comment