TANGAZO


Wednesday, December 9, 2015

Watu 5 wapigwa risasi na kuuawa Burundi


Image captionWatu 5 wapigwa risasi na kuuawa Burundi

Watu watano wamepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura.
Mauaji hayo ndio ya hivi punde zaidi kuwakumba waandamanaji wanaopinga muhula wa tatu wa urais wa Pierre Nkuruniza.
Miili yao ilipatikana ikiwa imepigwa risasi nyingi kando ya barabara ya kitongoji cha Cibitoke ambayo ni ngome ya vyama vya upinzani.
Walioshuhudia mauaji hayo wanasema kuwa waliwaona maafisa wa polisi waliotekeleza mauaji hayo wakiwasili kwa magari na kudai wanawasaka vijana waliowatupia guruneti.
Mwanamke mmoja aliyeshuhudia mauaji hayo aliiambia BBC kuwa mmoja wa wahasiriwa aliuiawa muda mchache tu baada ya kurejea nyumbani akitokea kazini.
Anadaiwa kuwa aliwaonyesha polisi kitambulisho chake cha kazini lakini hawakumsikiza.
Msemaji wa polisi naye anasema kuwa watano hayo waliuawa baada ya ufyatulianaji wa risasi uliotokea watlipowatupia polisi guruneti.

Image copyrightAFP
Image captionZaidi ya watu 200 wameuawa tangu rais Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu mwezi Aprili.

Polisi wawili walijeruhiwa huku watu wengine wawli wakiuawa katika kisa kingine kilichotokea usiku wa jana.
Maandamano yaliyoanza kwa vijana kupinga kauli ya rais Nkurunziza kuwania awamu ya tatu sasa yameanza kuchukua mrengo wa uasi dhidi ya uongozi wake.
Zaidi ya watu 200 wameuawa tangu rais Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu mwezi Aprili.

No comments:

Post a Comment