Watu 46 wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa katika shambulio la Taliban, katika uwanja wa ndege wa Kandahar Afghanistan.
Utawala nchini humo unasema kuwa raia 35 wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa .
Miili mingine 9 inaaminika kuwa ya wavamizi wa Taliban.
Duru zasema kuwa mwanamgambo mmoja angali ndani ya uwanja huo ambao ni makao makuu ya shirika la wanajeshi wa kujihami wa NATO, pamoja na jeshi la serikali ya Afghanistan.
Mashambulizi hayo yalianza Jumanne jioni pale wanamgambo wa Taliban wakiwa na silaha nzito nzito walipovunja ua na kuingia katika kambi hiyo.
Wapiganaji wengine wa Taliban walichukua udhibiti wa jumba moja refu mlimokuwemo shule na kulitumia kushambulia uwanja huo.
Mapema leo milio ya risasi ilisikika kutoka kwenye maeneo ambamo watu hao walikuwa wakizuiliwa.
Aidha wamebaini kuwa washambuiliaji wanazungumza ki-Urdu moja ya makabila yanayozungumzwa katika taifa jiranila Pakistan.
Serikali ya Afghanistan imekuwa ikiilaumu Pakistan kwa kudorora kwa usalama nchini humo na haswa katika maeneo ya Kandahar.
Abiria waliokuwa wanaelekea India wameshindwa kusafiri na huenda baadhi yao wametekwa na washambuliaji hao.
Taliban wanadai kuwa wamewauawa maafisa 80 japo idadi hiyo haijathibitishwa.
Lakini vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa huenda, idadi ya waliouwawa ikawa kubwa zaidi.
Mji wa Kandahar kwa muda mrefu umekuwa ngome ya kundi la Taliban.
No comments:
Post a Comment