Watu wa Venezuela wanapiga kura katika uchaguzi ambao unaonekana kuwa changamoto kubwa zaidi kukabili chama tawala cha Socialist, tangu chama hicho kushika madaraka miaka 17 iliyopita.
Viti vyote 167 vya bunge vinagombaniwa.
Venezuela ni kati ya nchi yenye mafuta mengi kabisa duniani, lakini uchumi sasa umezorota.
Kura za maoni zinaonesha kuwa raia wana kerwa na upungufu wa chakula na uhalifu unaozidi, na sasa wamevutiwa na ushirikiano wa vyama vya upinzani.
Hata hivyo Chama tawala bado kinaungwa mkono na wengi mashambani.
No comments:
Post a Comment