TANGAZO


Sunday, December 6, 2015

Jenerali Shwe 'amuunga mkono' Suu Kyi

Image copyrightAFP
Image captionKiiongozi wa zamani wa kijeshi wa Myanmar, Jenerali Than Shwe, na kinara mkuu wa upinzani nchini humo Bi Aung San Suu Kyi wamekutana
Kuna tetesi za kufanyika kwa mkutano wa siri kati ya kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Myanmar, Jenerali Than Shwe, na kinara mkuu wa upinzani nchini humo Bi Aung San Suu Kyi.
Mjukuu wa jenerali huyo ambaye anaaminika kuwa anaushawishi mkubwa nchini humo anasema kiongozi huyo wa chama cha NLD kilichopata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu mwezi uliopita anaweza kuiongoza taifa.
Mjukuu wa Jenerali Than Shwe, Nay Shwe Thway Aung ambaye alitumika kama muunganishi, amesema kwamba, jenerali huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 82 alimtaja Bi Suu Kyi kuwa kiongozi wa taifa wa siku zijazo, huku akisema kuwa atamuunga mkono.
Kupitia kwa ujumbe wa Facebook, Thway Aung alisema kuwa jenerali huyo ambaye ndiye aliyetekeleza kifungo cha nyumbani cha takriban miongo miwili u nusu alinukuliwa akisema kuwa
''nitaunga mkono jitihada zake''
Image copyrightEPA
Image captionMjukuu wa Jenerali Than Shwe, Nay Shwe Thway Aung ambaye alitumika kama muunganishi, amesema kwamba, jenerali huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 82 alimtaja Bi Suu Kyi kuwa kiongozi wa taifa wa siku zijazo, huku akisema kuwa atamuunga mkono.
Mkutano huo wao wa kisiri uliofanyika siku ya Ijumaa ulidumu kwa takriban saa mbili.
Juma lililopita viongozi wakuu nchini Myanmar wamekuwa wakijadiliana kuhusiana na swala kuu la urais.
Kwa mujibu wa katiba ya nchini Suu kyi hawezi kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa sababu anawatoto ambao wana uraia wa mataifa mengine.
Katiba hiyo iliundwa na utawala wa kiimla kwa nia ya kumfungia nje bi Suu Kyi.
Hata hivyo katika siku za hivi punde kiongozi huyo wa chama kilicho shinda cha NLD aliiambia BBC kuwa ndiye atakayemchagua rais mpya lakini hilo halitamzuia asichukue uongozi wa taifa hilo.

No comments:

Post a Comment