Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu Bw. Francis Nzuki akiongea na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
Wadau kutoka sehemu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
Mwakilishi kutoka Shirika linalohudumia Wazee (HELPAGE) na pia ni mshiriki Bw. Joseph Mbasha akiongea na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili malengo endelevu kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es salaam leo.
Wadau kutoka sehemu mbalimbali wakifatilia kwa makini hotuba iliyokua
ikitolewa na mgeni rasmi hayupo pichani wakati wa kongamano la kujadili malengo endelevu
kufikia malengo ya Milenia jijini Dar es Salaam leo.
Na Shamimu Nyaki-Maelezo
Dar es Salaam
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu duniani ambayo ni
tarehe10 Disemba mwaka huu,Tume ya haki za binadamu na Utawala bora leo
imeandaa kongamano la siku moja kujadili Mpango wa Maendeleo Endelevu unaotarajia kuanza rasmi januari mwaka2016.
Mgeni Rasmi
katika kongamano hilo Bi Rehema Ntimizi kutoka Tume ya haki za binaadamu
ameiomba jamii kushiriki kwa ukamilifu
katika kuleta maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla kwa kuwa maendeleo
yanaanza na watu wenyewe kwa kuhakikisha wanaondokana na umasikini,kuwa na afya
bora ,pamoja na elimu na kutambua kuwa ni haki yao kuwa na uwelewa wa suala
hilo.
“Binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa hivyo
wote tuwajibike katika maendeleo”Alisema bi Ntimizi.
Bi Rehema ameongeza kuwa dunia nzima kwa sasa
inashirikisha makundi yote katika jamii katika kutoa maamuzi hasa yale
yaliyosahaulika kama wanawake,wazee na watoto waishio vijijni hivyo wakati
umefika sasa kwa kila mtu katika jamii kushiriki hatua zote za maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano
la kujadili mpango huo leo jijini Dar es
salaam Mkurugenzi wa Tume ya haki za Binaadamu bw Francis Nzuki
ameeleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kujadili mpango huo wa maendeleo
endelevu jinsi gani utaleta matokeo
chanya katika kufikia malengo ya millenia ifikapo mwaka 2030.
Ameongeza kuwa mpango huo umejikita katika malengo kumi na
saba ambayo miongoni mwao ni kuondoa umaskini,kutoa Elimu bora, afya bora
pamoja na maji safi kwa kila kundi lililopo katika jamii ambao ni vijana,wazee,
wanawake, pamoja na watoto katika jamii ya Watanzania ili kuweza kufikia
malengo ya millenia.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa Tume itaanzisha
utaratibu wa kutembelea hospitali za
umma kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji ili kuweza kubaini malalamiko na
changamoto wanazopata wananchi ,lakini pia kutoa elimu jinsi watakavyoweza
kusaidiwa na tume pale wanakutana na changamoto katika suala linalohusu haki na
utu wao.
Kauli mbiu katika kongamano hilo ni “Haki zetu uhuru
wetu daima."
Aidha mshiriki kutoka shirika linalowahudumia wazee linaloitwa Helpage Intanational Fund Bw Joseph Mbasha amesema kuwa wazee wanapaswa
kushirikishwa katika masuala yote ya maendeleo kwa kuwa nao ni binaadamu na
wana uhuru wa kutoa mawazo na kupewa afya bora, kuondokana na umaskini lakini
pia kumiliki ardhi.
“Kila mmoja ashiriki katika maendeleo yake na Taifa
kwa ujumla.”Alieleza Mbasha.
Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa
haki za binaadamu wakiwemo Haki Elimu,YUNA,Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),Chuo kikuu cha Dar
es salaam pamoja na Chuo cha Uhasibu.
No comments:
Post a Comment