Mratibu wa Magonjwa ya Mlipuko Mkoa wa Dar es Salaam, Vicktoria Bulla (kulia), akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa afya wakati akifungua semina ya siku moja ya ugonjwa wa kipindupindu Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa mgeni rasmi. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma, Hellen Semu na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Janeth Mghamba. Semina hiyo iliandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Ofisa Habari wa Wizara ya Afyaaaa na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kulia), akibadilishana mawazo na mwenzake katika semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Mada mbalimbali kuhusu ugonjwa huo na magonjwa ya mlipuko zikiendelea kutolewa.
Semina ikiendelea.
Wadau wa Afya wakiwa kwenye semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wa jiji la Dar es Salaam asilimia 70 kati yao wanatumia maji yasiyo salama ambayo yanachangia kwa kiwango kikubwa kukithiri kwa magonjwa ya mlipuko.
Hayo yalibainishwa Dar es Salaam juzi na mtaalam wa afya kutoka idara ya kinga kitengo cha afya na mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Theophil Likingaga katika semina ya waandishi wa habari ya siku moja iliyoandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyohusu ugonjwa wa kipindupindu.
Dk. Likingaga alisema asilimia hiyo kubwa ya watanzania kutumia maji yasiyo salama imetokana na Shirika la Maji safi na Taka (DAWASCO), kuhudumia asilimia 30 tu ya wananchi wa Dar es Salaam hivyo kuwa changamoto.
Alisema pia asilimia 15 tu ya wananchu wa Dar es Salaam ndiyo waliounganishwa kwenye mfumo wa maji taka hivyo kyfanta tatizo la uhaba wa maji safi na utunzaji wa mazingira kuwa kubwa.
"Hayo ndiyo baadhi ya maeneo ambayo tumeyaona pia suala la uuzaji matunda kiholela, biashara za vyakula pia imekuwa ikichangia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu," alisema Dk. Likangaga.
Alisema wizara hiyo imejitahidi kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu kwa kugawa dawa za kusafisha maji pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Likangaga alisema serikali kupitia DAWASCO imejitahidi kufunga vioski katika maeneo mbalimbali na kusambaza maji kwa kutumia magari ili wananchi wapate maji safi na salama.
Kwa upande Mtaalam wa Maabara ya Taifa, Dk.Theophil Malibiche alisema tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze Agosti 15 mwaka huu, wamefanya vipimo 1071 ili kubaini vimelea vya kipindipindu.
Alisema kati ya hizo sampuli 668 sawa na asilimia 62 zimebainika kuwa na vimelea vya kipindupindu.
Kwa upande wake, Ofisa Afya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Emmanuel Mwandepa alisema serikali inaendelea kuangalia mbinu mbadala ya kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi.
Alisema kutokana na mkakati huo wameanzisha kampeni yq nyumba kwa nyumba ambayo itakuwa inakagua mazingira pamoja na ubora wa visima vya maji.
Aliongeza kutokana na mpango huo visima vifupi vya maji vitafungiwa ili kupunguza ugonjwa wa mlipuko.
(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment