Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ametakiwa Shirikisho la Soka Uingereza afafanue kuhusu matamshi aliyoyatoa kuhusu matumizi ya dawa za kutitimua misuli.
Wenger, mwenye umri wa miaka 66, wiki hii amenukuliwa akisema "mimi sijawahi kuwadunga sindano wachezaji wangu eti ndio wacheze vizuri zaidi „lakini kuna timu tumewahi kukutana nazo ambazo hazina mtazamo huu".
Alikuwa akizungumza wakati wa mahojiano ya L'Equipe baada ya mchezaji wa Dinamo , kufanyiwa uchunguzi wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu na vipimo vyake kupatikana na kasoro kufuatia ushindi wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Arsenal.
FA imemtaka Wenger awasilishe habari kuhudu madai hayo ambazo huenda labda anazo.
Vipimo vya kiungo wa kati Arijan Ademi vilipatikana na dosari hizo baada ya timu yake ya Dinamo kulaza Arsenal 2-1 mjini Zagreb. Sampuli zake zingine zingali zinachunguzwa na zikithibitishwa kuwa na kasoro huenda akapigwa marufuku.
Wenger amekuwa akitoa wito kuwe na mapambano makali dhidi ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu .
No comments:
Post a Comment