Makamu wa rais wa Shirikisho la Soka la Congo Jean Guy Blaise Mayolas na katibu mkuu wa shirikisho hilo Badji Mombo Wantete wamepigwa marufuku ya miezi sita na Fifa.
Lakini wawili hao tayari walikuwa wakitumikia marufuku za muda.
Hii ina maana kwamba watatumikia marufuku ya siku 45 pekee, ambazo ndizo zilizosalia ukiondoa siku ambazo wametumikia marufuku hiyo ya muda.
Mayolas na Wantete walipatikana na hatia ya kuvunja sheria za Fifa kuhusiana na “kutotoa na kupokea zawadi na marupurupu mengine”.
No comments:
Post a Comment