Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 127 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.
Watu 127 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea.
Wasimamizi wa mji wa Paris wamewataka raia kusalia manyumbani na wanajeshi 1,500 wametumwa kushika doria Paris.
Shambulio mbaya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kushikwa mateka.
Akiongea baada ya kufika katika ukumbi huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika watakabiliwa "bila huruma".
Mashambulio mengine yalitokea karibu na mighahawa ya Le Petit Cambodge na Le Carillon katika mtaa nambari 10 ambako mwandishi wa BBC anasema aliona watu 10 wakiwa wamelala chini, wakiwa wamejeruhiwa vibaya na wengine kufariki
- Moja kwa moja: Habari za karibuni zaidi kuhusu mashambulio Paris
- Bofya hapa kwa picha zaidi kuhusu mashambulio haya ya Paris
Mtu aliyeshuhudia ameambia gazeti la Liberation kwamba naye alisikia risasi zaidi ya 100 zikifyatuliwa katika mghahawa wa La Belle Equipe katika mtaa nambari 11.
Milio ya risasi pia ilisikika katika kituo cha kibiashara cha Les Halles.
Rais wa Marekani Barack Obama amelitaja shambulio hilo kuwa "jaribio lisilokubalika la kuhangaisha raia wasio na hatia" na kuahidi kusaidia Ufaransa kukabiliana na waliohusika.
"Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja," amesema.
"Tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia watu wa Ufaransa na mataifa kote duniani kuhakikisha magaidi hawa wanakabiliwa.”
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ameshtushwa sana na shambulio hilo na kuahidi kufanya "lolote tunaloweza kufanya kusaidia."
No comments:
Post a Comment