TANGAZO


Monday, November 9, 2015

Washiriki 20 wa shindano la Bongo Style waendelea kujifua

Washiriki wa shindano la Bongo style kwa upande wa picha wakimsikiliza kwa makini mtaalam wao Sameer Kermalli(wa tatu kulia) akitoa maelekezo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki kwa upande wa picha wakiwa wanasikiliza kwa makini somo.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande akiwa na washiriki wa shindano la Bongo Style ambao hawapo pichani, akiwa na Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alipofika kuwatembelea na kuongea nao machache.
Baadhi ya  Washiriki kwa upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanachakalika kuandaa kazi zao mbalimbali.
Mbunifu wa Mavazi Martini Kadinda akiwapa somo washiriki upande wa ubunifu wa mavazi.
Washiriki  wa ubunifu wa mavazi wakiendelea na kazi. 
Hawa ni washiriki kwa upande wa kupiga picha wakikamilisha moja ya mazoezi waliyopewa (Picha kwa hisani ya Washiriki upande wa wapiga picha)
Baadhi ya Washiriki upande wa kupiga picha wakiwa mtaani wakiwa katika mazoezi waliyopewa kuyafanya na mtaalam wao Sameer Kermalli.
Baadhi ya washiriki wengine kwa upande wa Kupiga picha  na ubunifu wa  mavazi wakisikiliza kwa makini somo ambalo linatolewa na mtaalam ambaye hayupo pichani.
Baadhi ya washiriki upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanasikiliza kwa makini maelekezo wanayopewa na Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda ambaye hayupo pichani.
Muda wa mapumziko. 
Muwezeshaji kutoka Wiki Loves Africa akitoa somo juu ya upigaji picha kwa washiriki ambao hawapo pichani.
Tunukiwa Daudi (Aliyesimama) akitoa somo juu ya matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na Faida zake.
Baadhi ya washiriki upande wa kupiga picha wakifurahia jambo

IKIWA  ni siku ya tano tangu Washiriki 20 wa Shindano la Bongo Style linalo andaliwa na asasi isiyo ya Kiserikali ya Faru Arts and Sport   Development Organization (FASDO), ikiwahusha Wapiga picha na wabunifu wa mavazi wenye umri kati 19-25 walioingia rasmi kambini tarehe  5.11.2015, ambapo tangu tarehe hiyo  washiriki hao  wameendelea kujifua zaidi huku wakipewa kazi mbalimbali za ubunifu na masomo mengine ikiwa ni sehemu ya shindano hilo. Wakiwa kambini washiriki hao wamepata nafasi ya kujifunza mambo mapya ambayo walikuwa hawayafahamu.


Fainali hizi zinatarajiwa kufanyika tarehe 27.11.2015 ndani ya ukumbi wa Alliance Francaise Jijini  Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa upande wa picha wamekili kuwa walikuwa wanaona kama wanafahamu vema kupiga picha lakini baada ya kupata somo wamegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu na mengine walikuwa wanayafanya lakini bila kujua kuwa walikuwa sahihi, Pia waliongeza kuwa wanashukuru kuwapata wataalam ambao wameweza kuwaonesha ni jinsi gani wanatakiwa kuwa wapiga picha wazuri.

Nao washiriki wa ubunifu wa mavazi wameshukuru kupata wataalam ambao wamekuwa wakiwapa maelekezo mengi ambayo  yalikuwa ni chachu kwao kwasababu kila mmoja kwa upande wake wamejifunza mambo mapya mengi na kuona kuwa kumbe sio lazima kuwa na ubunifu wa aina moja ya mavazi lakini wanaweza wakawa na aina nyengine nyingi kulingana na mazingira waliyopo na kuishukuru Fasdo kwa kuwakutanisha.

Mwalimu na mtaalam wa kupiga picha Sameer Kermalli amekili kuwa tangu darasa lianze washiriki hao wamekuwa na uelewa wa haraka na yeye kupata nafasi ya  kuwaelekeza mbinu mbalimbali za kupiga picha na kanuni mbambali za upigaji picha, washiriki hao wamekuwa wasikivu na wameongeza ubunifu zaidi jambo ambalo limemtia moyo mtaalam huyo.

Kwa upande wa Mbunifu wa mavazi Martin kadinda alisema kuwa washiriki wapo vizuri na kila mbunifu anakitu chake cha kipekee ambacho yeye anafanya mfano wapo wale ambao wanabuni nguo zao kwa kutumia kitenge tu, wengine wanatumia vitu vya asili, nguo za kisasa, nguo ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuvaliwa na zenginezo, aliwashauri kuwa wasiegemee katika kitu kimoja tuu au aina moja ya mavazi lakini wawe na ubunifu na kubadilika kila wakati kwa sababu mitindo inakwenda ikibadirika.

Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande  alipata nafasi ya kutembelea kambini na kujionea jinsi washiriki wanavyojituma katika kazi zao na maandalizi ya shindano hilo yanavyo kwenda.

"Ninachukua nafasi hii kwa niaba ya Fasdo kuwapongeza washiriki wote mliofanikiwa kuingia katika shindano hili la Bongo style ikiwa lengo ni kuwajengea uwezo zaidi wa kile ambacho mlikuwa mnafanya na sasa kipate kuwa zaidi" aliongea Chande na kuongeza kuwa kuna ushindani mkubwa na shindano linafuata vigezo vyote vya ushindani na washindi watakuwa wamekidhi vigezo hivyo.

No comments:

Post a Comment