TANGAZO


Friday, November 13, 2015

Vodacom yapeleka somo la Shule za Sekondari vijijini

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Vodacom,Tanzania wakiwa katika ofisi za Mkuu wa Shue ya Sekondari Shimbwe iliyopo kata ya Uru wilayani Moshi vijijini ambako walifika kwa ajili ya kujionea uwekwaji wa programu za kujifunzia katika Kompyuta mpakato zilizotolewa shuleni hapo na Vodacom.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali na Learning In sync Tanzania,Lisa Wolker akitoa maelezo kwa Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini Henry Tzamburakisi kuhusiana na Programu maalumu zilizowekwa katika Kompyuta mpakato zilizotolewa na Odacom.
Wafanyakazi wa Vodacom,Kana ya Kaskazini wakisikiliza kwa makini maelezo ya Lisa Wolker (hayupo pichani).
Baadhi ya Kompyuta zilizotolewa na Kampuni ya Vodacom kama msaada wa shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini.
Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini ,Henry Tzamburakisi akizungumza jambo na mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe, Jacob Costantine alipotembelea darasa la Kompyuta shuleni hapo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Learning Insync  akijaribu kuunganisha nyaya katika darasa la kompyuta lilopo shule ya sekondari Shimbwe iliyopo Uru wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakisi (kushoto) akiwa katika darasa la Kompyuta katika shule ya Shimbwe Sekondari ,wengine ni baadhi ya walimu katika shule hiyo ambao wamepatiwa mafunzo ya kompyuta.
Lisa Wolker akitoa maelekezo kwa walimu na wanafunzi.
Walimu na wanafunzi katika shule hiyo wakisikiliza kwa makini.
Mafunzo juu ya matumizi ya Programu maalumu ya kufundishia na kujifunzia yakiendelea katika darasa la Kompyuta katika shule ya sekondari ya Shimbwe.
Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Tzamburakisi akielekeza jambo kwa wananfunzi.

Jumla ya Kompyuta 30 zimetolewa na Vodacom kupitia mfuko wa Vodacom Foundation kwa shule ya sekondari Shimbwe ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa wataalamu wanao toa mafunzo ya matumizi ya Programu maalumu za kufundishia katika shule hiyo.
(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini)

No comments:

Post a Comment