Bw. James Mkuwa - Muhadhiri Msaidizi Idara ya uongozi wa Biashara CBE akitoa ufafanuzi kwa wageni mbalimbali kuhusu elimu ya Biashara wanayoitoa kwa wajasiriliamali ,wanafunzi ngazi ya shahada na cheti pia wale wanaotaka kufungua kampuni na BIashara kwa kuwapatia taaluma ili wajiandae kujiajili wenyewe.
Mmoja wa Wahitimu wa CBE aliyefanya vizuri katika fani ya Rasilimali Watu Bi. Happyness Onani akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Prof.Emmanuel Mjema.
Baadhi ya wanafunzi na wahitimu wakitembelea mabanda ya maonesho.
Picha na 6. Baadhi ya wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Zawadi na kwa wahitimu iliyofanyika CBE kampasi ya Dar es Salaam.
Wageni mbalimbali wakitembelea eneo la Vipimo na Mizani wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo na zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao katika Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam.
Na Aron Msigwa - MAELEZO.
13/11/2015.Dar es salaam.
TAASISI za elimu kote nchini zimeaswa kujenga utamaduni wa kuthamini na kutambua mchango wa wahitimu wanaofanya vizuri katika masomo yao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE) Prof.Emanuel Mjema wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti na zawadi mbalimbali wahitimu wa chuo hicho takribani 20 waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka 2015.
Akizungumza na jamii ya wanachuo na Wahitimu wa Zamani wa Chuo cha Elimu ya Biashara na wale wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini amesema chuo chake kina utamaduni wa kuwatuza wahitimu wanaofanya vizuri katika masomo yao kama motisha kuthamini juhudi zao ili kuhamasisha wengine kufanya vizuri zaidi.
Amesema wahitimu 20 wa fani mbalimbali zikiwemo za Rasilimali Watu,Uendeshaji wa Biashara, Ununuzi na Ugavi, Vipimo na Mizani, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Masoko na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ngazi ya Stashahada, Shahada,Diploma na Cheti wametunukiwa vyeti na kukabidhiwa zawadi mbalimbali.
Prof. Mjema ameongeza kuwa mbali na tuzo hizo wadau hao hususan wahitimu wa miaka ya nyuma wa chuo hicho wapata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kukijengea uwezo chuo hicho pamoja na kuangalia shughuli za kitaaluma zinazofanyika.
" Siku hii ni muhimu sana kwa Chuo cha Elimu ya Biashara, ni siku ambayo tunathamini wahitimu wetu waliofanya vizuri kwa kuwapa Zawadi za vtu mbalimbali kuthamini mchango na heshima waliokipa chuo chuo chetu" Alisisitiza Prof.Mjema.
Ameongeza kuwa utoaji wa zawadi na tuzo hizo unakwenda sambamba na na maadhimisho ya ya Mahafali ya 50 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam yatakayofanyika Novemba 12,2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mgeni rasmi atakua Rais mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hasani Mwinyi.
Akifafanua kuhusu mahafali hayo ya 50 amesema kuwa wahitimu wapatao 2050 wa ngazi mbalimbali watatunukiwa Shahada , Astashahada, Stashahada, shahada na stashahada za Uzamili.
Kuhusu suala la nidhamu chuoni hapo hasa mavazi amesema kuwa chuo chake kimeendelea kusisitiza nidhamu na kuweka kanuni zinazowabana wanafunzi huku akifafanua kuwa chuo hicho kilikua chuo cha kwanza kuweka sheria inayosimamia nidhamu ya mavazi kwa wanafunzi.
Amesisitiza kuwa mavazi ndiyo yanayompambanua mwananfunzi na kuonyesha tabia yake na kuongeza kuwa nidhamu inapokua juu inawapa wanafunzi fursa nzuri ya kupata ajira pindi wanapohitimu kwa kuwa tayari wanaaminika katika jamii.
Prof.Mjema amebainisha hali ya nidhamu ya mavazi inaendelea kuzingatiwa kutokana na Madhara ya kuzuiwanna kushindwa kuhudhuria vipindi wanayoyapata wanafunzi waliokuwa wanakiuka kanuni na taratibu za chuo hicho
"Vijana lazima wawe mfano wa kuiga na hawa ni wasomi ambao wanategemewa na taifa, CBE imeshafukuza wengi kwa kukosa nidhamu, pia mwanafunzi anayekosa maadili huathiri maendeleo ya chuo na wanafunzi wengine" Amesisitiza.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wa zamani wa chuo hicho (Alumnae) Bw.Lusekelo Mwandemange amesema kuwa wao kama wahitimu wanayo dhamana ya kuhakikisha maendeleo ya chuo hicho yanapatikana.
Amesema wahitimu hao wamekuwa kioo kwa jamii inayowazunguka kwa kuitumia elimu yao kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii
Aidha wameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki ya kuwawezesha wanafunzi wa chuo hicho katika fani mbalimbali kupata elimu yenye viwango ndani na nje ya nchi.
Pia wamesema kuwa wao kama wahitimu wameanzisha umoja wao utakaohusika kuchangia maendeleo ya chuo hicho
No comments:
Post a Comment