UNAMKUMBUKA yule dogo aliyeanzisha redio stesheni yake nyumbani kwao? Bila shaka umewahi kusoma story yake kwenye kijarida cha kila mwezi kiitwacho SHUJAAZ ambacho husambazwa na gazeti la Mwanaspoti na vibanda vya Coca Cola. Sasa hivi, dogo ana habari mpya na njema kwa vijana na wote wanaomfuatilia.
Nyota imeanza kung’ara upande wake na sasa redio kubwa Tanzania EAST AFRICA RADIO imeamua kumpa nafasi aweze kusikika hewani na show yake mpya iitwayo SHUJAAZ.
“Show yangu itahusika na lifestyle ya vijana kwa ujumla, bila kusahau burudani kali, story za wana mbali mbali wanaojituma na kutoboa katika kufikia malengo yao maishani.
Pia, utawasikia vijana mbali mbali wakijadiliana kuhusu ishu zinazowahusu, mfano PESA, MAPENZI, KAZI, MICHEZO, UJASIRIAMALI n.k, ni lazima tupeane mashavu kama vijana.” Alisema DJ Tee.
Show hiyo itakayoanza rasmi JUMAMOSI hii (07/11/2015) saa TISA alasiri, inatarajiwa kuvuta hisia za vijana wengi hasa wajasiriamali kwa kuwa itahusika na ishu zote ambazo zinawahusu vijana kama DJ TEE mwenyewe alivyoelezea.
Unaweza kupata maelezo zaidi kutoka kwake mwenyewe kwa kujiunga naye kupitia Facebook jina ni DJ Tee (http://on.fb.me/1FUl1hX), Twitter (http://bit.ly/1LLGEpK) na Instagram (http://bit.ly/1Hn07t4)
No comments:
Post a Comment