TANGAZO


Saturday, November 7, 2015

RIPOTI ZA MOJA KWA MOJA ZA LIGI YA UINGEREZA

RIPOTI ZA MOJA KWA MOJA ZA LIGI NCHINI UINGEREZA

5.02pm:Kocha wa Newcastle Steve McClaren aonekana pale akiwa ameridhika na bao lile moja
5.01pm:Bournemouth inatawala mchezo ikiwa na asilimia kubwa ya umiliki wa mpira lakini safu ya ulinzi ya Newcastle inakataa kufunguka ili kusawazisha.
4.45pm:Timu zote zinajaribu kuona lango la mwengine lakini bado safu zao za ulinzi zakataa
Kipindi cha pili Bournemouth 0 Newcastle 1
04:30pm Mchezaji Harry wa Bournemouth ampatia pasi safi Joshua King lakini refa aonyesha kibendera akisema ameotea.
04:23pm:Mkawaju wa Joshua King (Bournemouth) waokolewa .
04:20pm: Joshua King (Bournemouth) asababisha mkwaju wa adhabu.
Image copyrightGetty
Image captionNewcastle vs Bournemouth
04:19pm: Fabricio Coloccini (Newcastle United) apata mkwaju wa adhabu katika wingi ya kushoto.
04:16pm: Junior Stanislas (Bournemouth).Acheza vibaya hapa na kusababisha mkwaju wa adhabu
04:15pm: Vurnon Anita (Newcastle United) apata mkwaju wa adhabu katika wingi ya kulia..
04.11pm:Goooooooal Goal! Bournemouth 0, Newcastle United 1. MKwaju wa mguu wa kushoto wa Ayoze PĂ©rez (Newcastle United) kutoka katikati ya boxi wamuwacha kipa wa Bournemouth bila jibu
Jaribio jingine la mkwaju wa Andrew Surman [Bournemouth)
03:48pm Harry Arter (Bournemouth) apata mkwaju wa adhaby katika wingi ya kushoto.
3.45pm:Mechi kati ya Newcastle na Bournemouth
12.00:Ligi ya Uingereza
Image captionLigi ya Uingereza
Ligi kuu ya England itaendelea kutimua vumbi leo kwa nyasi za viwanja saba kuwaka moto.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Chelsea wenye mwendo wa kusuasua watakua ugenini katika dimba la Britannia kuwakabili Stoke City.
Manchester United watakua katika uwanja wao wa Old Trafford kuwalika West Bromwich Albioni.
Wagonga nyundo wa london West Ham watawaalika The Toffees Everton, huku paka weusi wa Sunderland wakiwakaribisha watakatifu wa Southampton katika uwanja wa Light.
Michezo mingine ni
Bournemouth na Newcastle
Leicester na Watford
Norwich na Swansea

No comments:

Post a Comment