TANGAZO


Friday, November 13, 2015

Rais Magufuli ashiriki Ibada ya Misa ya kumuombea marehem mjukuu wake

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo wakati wa ibada ya msiba ya mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose Mlyambina (8) iliyofanyika huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo na kisha mwili wa marehemu kusafirishwa kwenda Geita kwa mazishi.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwafariji wazazi wa Marehemu Jose Mlyambila na Suzan wakati wa ibada ya mazishi ya mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose Mlambila huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwafariji wazazi wa Marehemu Jose Mlyambila na Suzan wakati wa ibada ya mazishi ya mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose Mlambila huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janet Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza la mjukuu wao marehemu Maryfaustina Yose Mlyambina (8) wakati wa ibada ya msiba iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu Temboni Kimara jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la mjukuu wa Rais John Pombe Magufuli marehemu Maryfaustina Yose Mlyambina aliyefariki akiwa na umri wa miaka nane baada ya kuugua. Ibada misa ya kuuombea marehenu na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janet Magufuli(wapili kulia), Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassani Suluhu (wapili kushoto), Rais Mstaafu awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Said Meck Sadik wakiwa katika ibada ya kuuombea marehemu mjukuu wa Rais John Pombe Magufuli marehemu Maryfaustina Yose Mlyambila iliyofanyika nyumbani kwa wazazi ya marehemu Kimara Temboni jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Freddy Maro). 

No comments:

Post a Comment