TANGAZO


Thursday, November 12, 2015

Msumbiji na Zambia zashinda

Image copyrightReuters
Image captionTimu ya taifa ya Zambia
Timu za taifa za Msumbiji na Zambia zimepata ushindi katika kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia nchini Urusi 2018.
Timu hizo zimepata ushindi katika mchezo wa raundi ya pili.
Msumbiji walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gaboni, katika mchezo uliochezwa jijini Maputo, bao pekee likufungwa na mshambuliaji Helder Pelembe.
Gabon wenyeji wa michuano ya mataifa ya mwaka 2017 walicheza mchezo huo bila ya nyota wao Pierre-Emerick Aubameyang, anayesumbuliwa na maumivu.
Mchezo wa marudiano wa timu hizi mbili utafanyika siku ya Jumamosi katika mji wa Libreville.
Zambia wakiwa ugenini katika dimba la Karima walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan, mshambuliaji Winston Kalengo ndie aliyeipa ushindi Chipolopolo katika dakika ya 28 ya mchezo.
Zambia watakua wenyeji wa Sudan katika mchezo wa marudio utakaofanyika mjini Ndola siku ya jumapili.

No comments:

Post a Comment