Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za CUF, Mtendeni kuhusiana na maendeleo ya “mkwamo” wa kisiasa Zanzibar. (Picha zote na Salmin Said, OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za CUF, Mtendeni kuhusiana na maendeleo ya “mkwamo” wa kisiasa Zanzibar.
ZANZIBAR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za CUF, Mtendeni kuhusiana na maendeleo ya “mkwamo” wa kisiasa Zanzibar.
ZANZIBAR
Na Hassan Hamad (OMKR)
MAKAMU wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema jitihada za kuutafutia
ufumbuzi mkwamo wa kisiasa Zanzibar uliotokana na tamko la Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi Zanzibar Bw. Jecha Salim Jecha baada ya kutangaza kufuta uchaguzi uliofanyika
tarehe 25 Oktoba 2015, zinaendelea vizuri.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika ofisi za CUF Mtendeni mjini Zanzibar jana, Maalim Seif
ambaye pia ni mgombea Urais kupitia Chama hicho amesema ana matumaini kuwa
suala hilo litapatiwa ufumbuzi wa haki unaoheshimu maamuzi ya wapiga wa
Zanzibar waliyoyafanya tarehe 25 mwezi uliopita.
Amefahamisha kuwa
jitihada hizo zimekuwa zikifanywa na taasisi mbali mbali za ndani na nje ya
nchi zikiwemo Umoja wa Mataifa pamoja na nchi kadhaa ambazo ni marafiki wa
Tanzania zikiwemo zilizoleta waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi huo.
Amesema jitihada pia
zimekuwa zikifanywa na viongozi wakuu wastaafu, viongozi wa dini na Msajili wa
vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi.
Ameeleza kuwa Chama
Cha Wananchi CUF kimetiwa moyo na imani kutokana na jitihada hizo, na kwamba
ufumbuzi wa haki wa suala hilo utapatikana katika kipindi kifupi kijacho.
Maalim Seif ametumia
firsa hiyo kuwataka Wazanzibari waendelee kubaki watulivu na kuitunza amani ya
nchi, na kuwaaachia viongozi wao kulifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na
watu mashuhuri pamoja na Taasisi za kitaifa na kimataifa.
Amewaomba wakuu wa
vyombo vya ulinzi na usalama kufanya juhudi kuhakikisha Zanzibar inabaki katika
hali ya amani na utulivu, na kutokubali kutumiwa na wanasiasa kufanikisha mbinu
chafu ambazo zinaleta taharuki na hofu miongoni mwa raia.
Maalim
Seif amewahakikishia viongozi na wanachama wa CCM na Wazanzibari wote kwamba iwapo
atatangazwa mshindi wa uchaguzi huo hakutokuwa na ulipizaji wa kisasi, na
kwamba atafanya kazi kwa ushirikiano chini ya muundo wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa kwa maslahi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment