Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez
Dar es Salaam, Novemba 09, 2015:
KAMPUNI ya simu ya Tigo imewaomba radhi wateja wake kutokana na kukatika kwa huduma zake katika sehemu nyingine nchini jana.
KAMPUNI ya simu ya Tigo imewaomba radhi wateja wake kutokana na kukatika kwa huduma zake katika sehemu nyingine nchini jana.
Taarifa ya
kampuni hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam imesema
kukatika kwa huduma za Tigo “kulitokana na sababu zilizo nje ya uwezo kwa kampuni
zilizo tokana na kukatika kwa mkongo sehemu tofauti tofauti.” Aidha taarifa hiyo
iliendelea kusema kwamba “tatizo hilo sasa limeshughulikiwa kikamilifu na huduma
zote za Tigo zimerejea katika hali yake ya kawaida.’’
“Tuna sikitishwa
na usumbufu uliojitokeza kutokana na kukatika kwa huduma zetu natunapenda kuwahakikishia
wateja wetu dhamira ya kampuni yetu kuendelea kuwapa wateja huduma zenye ubora wa
hali ya juu, za kutegemewa na kwa gharama nafuu,” amesema Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.
Aidha Gutierrez
ametoa shukrani kwa wateja wa Tigo kwa uvumilivu wao na kutangaza kwamba kama ishara
ya kuomba msamaha kampuni ina wapa wateja wake wote dakika 10 za muda wa maongezi,
SMS za bure kwenda mtandao yote na 10mb za kuperuzi Intaneti kwa siku nzima ya leo.Kifurushi
hiki mteja ana kipata kwa kutuma neno BURE kwenda namba 15304.
No comments:
Post a Comment