Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo.
|
Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio.
|
Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge.
|
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo.
|
Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia.
|
Wengine walitishia kujinyonga mbele yake.
|
Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge.
|
Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zile tulizozizoea.
|
Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,Elzabeth Minde aliingilia kati kujaribu kuomba Mosha kubadili uamuzi wake huo bila ya mafanikio.
|
Wanaccm wengine walilazimika kupanda jukwaani bado walizuiliwa.
|
Wengine walizimia na kupatiwa msaada wa huduma ya kwanza.
|
Mosha aliondolewa uwanjani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi kutokana na wanachi walioonekana kutofurahishwa na uamuzi wake huo.
|
Msafara wake ulisindikizwa na askari Polisi. (Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini)
|
No comments:
Post a Comment