Algeria ilifunga kwa mara ya pili katika dakika ya tano za mwisho na kusajili ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Lesotho katika michuano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
Faouzi Ghoulam alifikisha Algeria katika ngazi ya juu katika dakika ya 31 lakini baada ya dakika sita wenyeji wakafunga bao la kusawazisha kupitia kwa Ralekoti Mokhahlane.
Dakika ya 85 El-Arbi Hilal Soudan airudisha timu ya Algeria kifua mbele dakika chache kabla mchezo kukamilika.
Ushindi huo umerudisha Algeria juu ya jedwali katika kudi J huku Lesotho wakisalia mwisho bila alama yoyote.
Mabingwa Ivory Coast walicheza mechi yao ya ufunguzi kwa kutoka sare na timu ya Sierra Leone.
Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Port Harcourt,Nigeria .
Sierra Leone bado wamepigwa marufuku ya kuwa wenyeji wa mechi za kimataifa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Ilikuwa mwanzo mbaya kwa Michel Dussuyer tangu kung'atuka mamlakani kwa kocha wa Elephant's.
Kwa upande wake walimkosa kiungo Yaya Toure ambaye alikuwa amekataa kuchukuliwa akidai anatathmini hatima yake katika michezo ya kimataifa.
Mshambulizi wa Zamalek Bosem Morsy alifungia timu yake ya Misri mabao matatu kwa na kuisaidia kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Chad katika kundi G.
Nigeria wana pointi mbili nyuma baada ya kutoka sare nchini Tanzania siku ya jumamosi.
Cameroon waliwachapa Gambia 1-0 huko Banjul na kuongoza katika kundi M.
Mabigwa wa 2012 Zambia walitoka nyuma na kuibana Harambee stars ya Kenya mabao 2-1 katika kundi E.
Matokeo ya Afcon
Sierra Leone 0-0 Ivory Coast
Madagascar 0-0 Angola
CAR 2-0 DR Congo
Mauritius 1-0 Msumbiji
Swaziland 2-2 Malawi
Lesotho 1-3 Algeria
Zimbabwe 1-1 Guinea
Chad 1-5 Misri
Kenya 1-2 Zambia
Benin 1-1 Mali
The Gambia 0-1 Cameroon
Libya 1-2 Cape Verde
No comments:
Post a Comment