Mwanamke mmoja wa kipalestina amekufa kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa shambulio mwezi Julai lililomuua mumewe na mtoto wao mdogo wa kiume.
Riham Dawabsha alikua anauguza majeraha ya kuungua kiasi cha asilimia tisini ya mwili wake aliyoyapata baada ya nyumba yao kupigwa na mabomu ya moto katika kijiji cha Duma kilichopo katika ukingo wa magharibi .
Shambulio hilo linaaminiwa kufanywa na walowezi wa kiyahudi.
Mtoto wake wa miezi 18 aliuawa katika shambulio hilo pamoja na mumewe ambaye alikufa hospitalini wiki moja baadaye .
Mtoto mwingine wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne bado anapata matibabu ya majeraha.
Shambulio hilo lililaaniwa na jamii ya kimataifa na kusababisha maandamano makubwa ya wapalestina
Maafisa wa polisi nchini Israeli waliwakamata watu 7 wanaoshukiwa kuvamia nyumba hiyo ya mpalestina katika ukingo wa magharibi na kuiteketeza moto.
No comments:
Post a Comment